Friday, 9 August 2013

RAY C AENDELEA KUSIMULIA JINSI ALIVYOSHAWISHIWA KUVUTA BANGI NA MADAWA MENGINE ( SEHEMU YA MWISHO)

Kipande cha mwisho cha kipindi cha The Interview cha Clouds TV ambapo kilihusisha mahojiano na mwanamuziki Rehema Chalamila aka Ray C kilirushwa jana usiku.

Katika sehemu hiyo Ray C alizungumzia jinsi ilivyokuwa ngumu kwake kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya, wasanii wengi walivyoingia kwenye janga hilo na jinsi Tanzania ilivyoathirika na madawa hayo.

“Hali ni mbaya, wasanii wengi, wengi sana wameingia, sitaki kujua wameingiaje lakini najua kama nilivyoingizwa nao wameingizwa hivyo. Kwamba wasanii ‘aah anaimba tu pale anapata milioni tano, yaani msanii hana kazi anapiga piga tu yoyoyo, kashapata pesa.

“Kwahiyo pesa zao si za mwisho wa mwezi, lisaa limoja kaimba kashapata pesa. Kwahiyo wanafuatwa wale, tuwaingizie ili na wao wakishakuwa maaddict pesa zao zote wanazopata tutazipata sisi.

“Kwahiyo usishangae wasanii wengi wameingia lakini najua wameingizwaje, kwa style hiyo. Kwahiyo ni wengi sana sasa hivi, si wa filamu, si wanamuziki,” alisema.

“Addiction si kwa wasanii tu. Kuna watu wanakuja na tai nzuri anaonekana yeye anafanya kazi benki kumbe akitoka hapo anaenda anapona halafu anarudi.Kwahiyo ni kila Mtanzania yeyote, Watanzania tumeumia,” alisisitiza.

“Si watoto wa shule, si wasanii, si watu wazima na tai zao. Huu ni ugonjwa, ni ugonjwa kama ugonjwa mwingine. Addiction is a disease like any other disease.

“We si una Malaria? Hata mimi si ni addict? Mimi pia naumwa. Kwahiyo mimi mwenyewe nikienda Muhimbili pale nasema I am an addict, I am sick, ukisema an addict ni kwamba you are sick.

“Watu wengi wana mentality kwamba ‘huyu amejitakia mwenyewe’. Sio, ni ugonjwa, akishaingia ameumia akitaka kutoka anashindwa.

“Kwahiyo ni ugonjwa kama ugonjwa mwingine na unatibika kama ugonjwa mwingine. Kwahiyo mimi nimeenda Muhimbili kama mgonjwa, nimewaambia tatizo langu ni hili madaktari wa akili, madaktari wa sijui hivi wamenitibu mimi nimepona kama mgonjwa mwingine, addiction is a disease.

“Mimi na madawa sikujitakia, haujui nimeingiaje ndugu yangu usiniseme mimi mwenyewe nataka kutoka nashindwa. Naamka asubuhi miguu inaniuma.

Naumwa kama mtu wa kansa. Viungo vyote vinaniuma, nafanyeje? Nipate kidogo ili nipone lakini si kwamba napenda.”

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...