Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’.
STAA wa filamu na muziki Bongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ amekiri
kuwa katika wakati mgumu kutokana na kukabwa na mashetani usiku na
kumsababishia maumivu makali ya mwili hadi kuhisi kufa. Hivi karibuni Jini Kabula alipotea kwenye ulimwengu wa mastaa jijini
Dar hivyo Ijumaa Wikienda likaamua kumtafuta, alipopatikana ndipo
likabaini hali yake ni tete kiafya.Akizungumza na mwanahabari wetu wikiendi iliyopita, Jini Kabula alisema kwa muda mrefu sasa amekuwa mtu wa kuumwaumwa na mwili kukosa nguvu ambapo alishapima vipimo vyote lakini aligundulika kuwa na malaria, akatumia dozi na kuimaliza lakini hali bado siyo nzuri. Huku akiwa amedhoofu mwili, Jini Kabula alisema kila ikifika usiku wa manane akiwa amelala huwa anakabwa na mtu ambaye hamuoni, hali inayomfanya ashindwe kupumua huku mwili ukikosa nguvu na kuuma kupindukia. |
“Hata rafiki zangu nimeshawaaga na kuwaambia kuwa muda wowote wakisikia nimekufa wasishangae kwa sababu naumwa ila ninayemhurumia ni mwanangu, jamani nitamuacha bado mdogo maskini wa Mungu sijui ni shetani gani ametukumba wasanii,” alisema Jini Kabula kwa masikitiko.
Credit GPL
No comments:
Post a Comment