HAWA JAMAA NDIO WAMEVUNJA REKODI KWA KUIZUNGUKA DUNIA KWA KUTUMIA HII BAJAJI...KUMBE WALIFIKA MPK BONGO NA KIBAJAJI:
Watanzania
wengi tunafahamu Bajaji ni usafiri wa hapa na pale tu, yani sio
usafiri wa kubeba abiria kwenye masafa marefu lakini Walimu wawili raia
wa Uingereza wamekipiga kibajaji gia na kupita nacho nchi mbalimbali
duniani zinazofikia 37.
Ni safari ambayo wameianza August 13
mwaka jana (2012) lakini haijafikia hapa bila matatizo, wanakwambia
Bajaji imezingua sana kwenye baadhi ya nchi na kuna wakati injini
ilisumbua wakajua ndio mwisho wa safari mpaka wakati mwingine
wanalazimika kushuka na kuanza kuivuta wao wenyewe.
Unaambiwa hii rekodi itaingia kwenye
kitabu cha Guiness kama watamaliza safari yao ambayo wamepanga
kuimalizia Brazil kabla ya December 23 2013 kisha kurudi zao nyumbani
Uingereza.
Wanasema wengine wameshindwa kuamini
kama wanaizunguka dunia kwa ‘tuktuk’ a.k.a Bajaji ambapo kwenye mpaka
wa Kenya na Uganda walisimamishwa na Polisi ambae aliwaambia haamini
kuhusu urefu wa safari yao ila kama ni kweli, itakua ngumu wao kupata
watoto wa kiume.. labda wa kike.
Wakiwa South Africa.
Wakiwa Paris.
Wakielekea kwenye mpaka wa Hispania.
Barcelona Hispania.
Wakizungumza na Wanafunzi Ethiopia.
Hapa kwenye picha ya juu ni Burundi.
Hapa kwenye vumbi, wameandika ni Magharibi mwa Tanzania.
Ni safari ambayo haijakwenda bila kasoro, hapa ni Northern Peru.
No comments:
Post a Comment