DUH! Ule mwaliko wa wasanii wa Bongo Muvi kwenda Ikulu kwenye futari kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, umeota mbawa baada ya kuambiwa ‘msije’ hivyo kusababisha baadhi ya mastaa waliokusanyika kuumbuka.
Ishu hiyo ilitokea mwanzoni mwa wiki hii ambapo mastaa hao walipata mwaliko huo wa kutakiwa kwenda Ikulu kufuturu na JK baada ya wale wa Bongo Fleva.
UJIO WA CLINTON
Habari zilidadavua kuwa chanzo cha kutoswa kwa mastaa hao ni kufuatia ujio wa Rais Mstaafu wa 42 wa Marekani, Bill Clinton.
Wakiwa tayari wamelipuka ‘madela’ na ‘makanzu’ kwa ajili ya kwenda kugonga mnuso na ‘mkubwa’ na kuzungumza naye, ghafla mambo yalibadilika na kujikuta wakiwa wamenunaje?
WAKOPA MADELA, KANZUUJIO WA CLINTON
Habari zilidadavua kuwa chanzo cha kutoswa kwa mastaa hao ni kufuatia ujio wa Rais Mstaafu wa 42 wa Marekani, Bill Clinton.
Wakiwa tayari wamelipuka ‘madela’ na ‘makanzu’ kwa ajili ya kwenda kugonga mnuso na ‘mkubwa’ na kuzungumza naye, ghafla mambo yalibadilika na kujikuta wakiwa wamenunaje?
Habari za chini ya kapeti zilidai kuwa baadhi ya mastaa hao walikuwa wamekopa madela na makanzu hivyo kusitishwa kwa mwaliko huo kuliwauma kupita maelezo kwani walikuwa tayari kwa kuuza sura na JK.
Huku Ijumaa likiwachabo kila ‘step’, mastaa hao walikubaliana kukutana pamoja kwenye Viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini Dar kwa ajili ya kuanza safari ya kuelekea Ikulu huku kila mmoja akisisitizwa kuwa ‘smati’.
Kwa upande wa mastaa wa kiume walinunua na wengine kukopa kanzu za gharama huku upande wa wanawake wakiwa wametinga madela yao maalum ya gharama tayari kwenda kupata futari ‘White house’.
KIKAO CHA DHARURA
Wakiwa wamekusanyika viwanjani hapo kama wanavyoonekana pichani, ilipofiki saa 11:30 jioni, aliyekuwa Katibu wa Bongo Movie, Salum Mchoma Chiki ghafla alisimama na kuwaomba wasanii wasogee kwa pamoja kwani kulikuwa na kikao cha dharura.
WAKATWA MAINI
Walipokusanyika, Chiki alipaza sauti na kusema: “Jamani tuliokuwa tunakwenda kwa Mheshimiwa Rais kwa ajili ya kufuturu, safari hiyo haipo tena kama tulivyokuwa tumejuzana.”
Kauli hiyo iliwakata maini mastaa hao ambao wote walionekana kunywea huku wakitia huruma.
Chiki aliendelea: “Safari yetu imekatishwa na ugeni alioupata Mheshimiwa Rais lakini bado tutajulishwa ni siku gani ya kwenda kufuturu naye.”
Maneno ya Chiki yaliendelea kuwasononesha wasanii hao huku wengine wakiangua kicheko, kila mmoja akimuangalia mwenzake alivyojipigilia nguo za maana.
STEVE NYERERE
Komediani Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ aliweka maneno ya utani kwa kusema kwa wale waliojitundika dela lakini halikumkaa vizuri au kama alikopa na hajalipa, ndiyo ulikuwa muda mzuri wa kujipanga zaidi hivyo wasisononeke.
WATIWA MOYO
Alisema: “Jamani kama mlibandika madela, msijali kabisa huu ndiyo muda muafaka wa kujipanga zaidi na kulipa madeni ambayo mlikuwa nayo kutokana na viwalo mlivyovaa leo.”
LULU, MAMA KANUMBA
Baadhi ya mastaa ambao walionekana kujipigilia na kupendeza tayari kwa kwenda Ikulu kabla ya mambo ‘kuharibika’ ni pamoja na Elizabeth Michael ‘Lulu’ ambaye alitimba na mama wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa.
Jacob Steven ‘Jb’, Mohamed Nice ’Mtunisi’ na Ben Kinyaiya wakiwa wametinga makanzu mapya nao walikuwa wamelipuka vilivyo.
WAONDOKA WAKIWA WAMENUNA
Baada ya taarifa hiyo chungu kwa mastaa hao, kila mmoja aliondoka viwanjani hapo akiwa amenyong’onyea.
Badala ya Jumamosi, kuna habari kuwa walitakiwa waende siku inayofuatia (Jumapili) lakini nayo ikashindikana na kusemekana itakuwa Jumatatu ambayo nayo pia hawakwenda hadi ratiba za kufuturisha Ikulu zikamalizika, wakipewa moyo kwamba labda itakuwa mwakani.
No comments:
Post a Comment