Friday 9 August 2013

AFYA YA MSANII MATUMANI IMEIMARIKA KIDOGO NA AMEREJEA TENA KATIKA FANI YAKE YA UIGIZAJI


BAADA ya kutoka nchini Msumbiji akiwa hoi, msanii wa vichekesho Bongo, Tumaini Mwakibibi ‘Matumaini’ hatimaye amepata nguvu na ameanza kujikongoja katika kazi ya uigizaji.
 
Akiongea na  mwandishi  wetu hivi karibuni, Matumaini alisema kwa sasa anaendelea vizuri na ameshaanza kucheza filamu mbalimbali anazoshirikishwa na wasanii wenzake na sasa anaendesha maisha yake mwenyewe.
  
“Nawashukuru sana wasanii wenzangu kwani kama siyo wao, ningerudishwa nikiwa maiti, sina cha kuwalipa ila Mungu ndiye atakayewalipa,” alisema Matumaini.
 
Hata hivyo, alilaani vikali baadhi ya wasanii wanaozusha maneno ya uongo kwamba Michael Sangu alikula fedha alizokuwa anachangisha kwa ajili yake jambo ambalo siyo la kweli

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...