Tuesday 18 June 2013

BAADA YA TID KUMPIGA MKWARA OMMY DIMPOZ, SASA OMMY AAMUA KUJIRUDI SOMA HAPA

SIMU chache baada ya Msanii wa Bongo Fleva Khalid Mohamed (T.I.D) aka Mnyama atangaze kuwa anamsaka msanii mwezake wa muzi, Omar Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’, kwa kosa la kumdhihaki na kumtusi mtu aliyetangulia mbele za haki Albert Mangwea,msanii huyo amejitokeza hadharani na kuomba radhi.
Juni 8, mwaka huu, katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, wakati wa utoaji wa Tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards (KTMA) mwaka 2012-2013, Ommy Dimpoz alisema kwamba kamwe hawezi kufa maskini kama alivyokufa msanii mwenzake Albert Mangwea.
Kwa kutambua kwamba kauli hiyo iliudhi wadau mbalimbali wa muziki wake,Omy Dimpozi ameamua kuuangukia umma na familia ya marehemu Mangwea na kuomba msamaha.
Akizungumza na Mwanadishi waHabarimpya.com Msanii huyo alisema kwamba anakwenda kuiomba msamaha familia ya marehemu na baada ya hapo atarudi kuwaomba msamaha watanzania wote kwa kupitia baadhi ya vyombo vya habari.
“Samahani sana mashabiki wangu nakubali mimi ni mtu na bila ninyi sitaweza kufanya lolote lile,na sikuongea kuhusu Legend Ngwea kwa hila mbaya. One love”alisema Omy Dimpozi.
Msanii huyu aliamua uamuzi wakuomba msamaha baada ya kuona mashabiki wengi na baadhi ya wasanii kuchukia na kutangaza kumtembezea kichapo wasanii waliopanga kumtembezea kichapo ni pamoja na Khalid Mohamed(TID).
"Hawa watoto wadogo wanakuja na kandambili kuomba kuimba sasa hivi wanajifanya wao wanazo hela sana na kututusi sisi especially mkali wangu Albert wallahi mungu ...”alisema TID.
"Hawa watoto wadogo wanakuja na kandambili kuomba kuimba sasa hivi wanajifanya wao wanazo hela sana na kututusi sisi especially mkali wangu Albert wallahi Mungu ...”alisema T.I.D, T.I.D alisema kwamba anamsaka msanii huyo na akimpata atampa kichapo kikali kutokana na kauli yake ya kumpa kashfa msanii aliyetutangulia mbele za haki.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...