Friday, 3 May 2013

BREAKING NEWZZ : MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2012 KUSAHISHWA UPYA

 
TAARIFA  KUTOKA BUNGENI MUDA HUU AMBAPO WAZIRI LUKUVI  AMETANGAZA KURUDIWA UPYA KUSAHISHWA KWA MITIHANI YA KIDATO CHA NNE KWA MWAKA 2012,HII IMETOKANA NA MAPENDEKEZO YALIYO TOLEWA NA TUME ILIYO UNDWA KUCHUNGUZA TATIZO LA WANAFUNZI WENGI KUFELI KATIKA HUO MTIHANI,PIA AMESITISHA KUANZA KUTUMIKA KWA VIWANGO VIPYA VYA UFAULU.
Habari kutoka bungeni ni kwamba matokeo yote ya  kidato  cha  nne yamefutwa na yatasahihishwa upya haraka iwezekanavyo..
 
Taarifa ya tume iliyoundwa na waziri mkuu kuchunguza sababu za kufeli vibaya kwa watajiniwa wa form 4  imesomwa  bungeni  leo  na  mh.LUKUVI. 
LUKUVI amesema sababu zilizosababisha  wanafunzi  wafeli   ni upungufu wa waalimu, mazingira magumu a kufundishia, idadi kubwa ya shule za sekondari iliyopelekea idadi kubwa ya watahiniwa  na  utaratibu  mbovu  wa  baraza  la  mitihani  uliotumika  bila  kuwashirikisha  wadau  wa  elimu
Mh.  LUKUVI amesema kuwa NECTA haikufuata vigezo vya kuwafaulisha wanafunzi kwa kufuata STANDARDTIONS na CONTINOUS ASSESMENTS. ...
Hivyo  basi, matokeo  hayo  YAMEFUTWA  na  YATASAHIHISHWA  UPYA

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...