DIVA wa
filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameziomba mamlaka
zinazosimamia maadili ya filamu nchini ziwaruhusu wasanii waigize nusu
utupu ili kuendana na soko la kimataifa.
Akitetea
hoja yake mbele ya paparazi wetu, staa huyo aliyeitendea haki filamu ya
Foolish Age alitolea mfano Tamthiliya ya Shuga iliyomtoa Lupita Nyong’o
ambayo alicheza akiwa nusu utupu.
“Wanasema
hatufuati maadili wakati kuna muvi ambazo zipo theatre na watu
wanaangalia hazina maadili, wao wanataka tufanye vitu kwa kudanganya
wakati sasa hivi tuko dunia ambayo tuna takiwa tuweke vitu wazi,
wasibane sana,” alisema Lulu
No comments:
Post a Comment