Mwanamuziki Rehema Chalamila ‘Ray C’, ametoka katika Hospitali ya Mwananyamala, Dar es Salaam alikokuwa amelazwa.
Mwanamuziki huyo ambaye amekuwa katika tiba ya kuachana na matumizi ya
dawa za kulevya hospitalini hapo, alifikishwa hapo juzi Jumatatu asubuhi
na baadhi ya madaktari walibainisha kuwa Ray C alikuwa anasumbuliwa na
ugonjwa wa dengue ambao umelipuka katika maeneo mengi jijini Dar es
Salaam hivi karibuni.
Akizungumza kwa simu jana, Ray C alisema ameondoka hospitalini na yuko nyumbani baada ya kuruhusiwa na madaktari.
Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dk Sophinias Ngonyani alisema mwanamuziki
huyo aliruhusiwa baada ya kupata nafuu na hali yake kuonekana nzuri.


No comments:
Post a Comment