Saturday, 4 January 2014

WATU 9 WAPOTEZA MAISHA KWENYE TUFANI YA THELUJI ILIOANGUKA MAREKANI KATIKA MIJI YA DMV,PA, NY, CT NA MA


Pendera ikionekana imechanika kwenye ufukwe wa Scituate Massachusetts baada ya tufani ya theluji iliyoanguka siku ya alhamisi Jan 2, 2014 na kusababisha vifo vya watu 9 mji wa Boston imeanguka theluji ipatayo futi 2 na kusababisha kufunga barabara kuu inayounganisha Pennsylvani, New York na Boston, viwanja vya ndege, Mssachusetts, New York vilisitisha safari za ndege mpaka hapo theluji itakapokwanguliwa na hali kuwa salama kwa ndege kuruka. Meya wa New York ilibidi atangaze hali ya dharura (State of Emergency) kwa wakazi wa jiji hilo lisilolala. Picha na Michael Dwyer
mpiga picha akipata ukodak moment kwa sananmu iliyotengenezwa kwa theluji karibu na Capitol Hill mjini Washington, DC. ambapo theluji ilianguka ipatayo inchi 3 mpaka 5 kwa maeneo mengine ya Virginia na Maryland. picha na Evan Vucc
Daraja la RFK New York lilivyokua likionekana siku ya Ijumaa Jan 3, 2014 baada ya theluji kuanguka siku ya alhamis jioni na kusababisha shule na ofisi za serikali kufungwa. Picha na John Minchillo
Watembea kwa miguu wakivuka barabara siku ya alhamisi kwenye jiji lisilolala la New York wakati theluji ilipokua ikidondoka. picha na John Minchillo
Maeneo ya Time Square yalivyoakua yakionekana wakati theluji ilivyokua ikianguka

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...