RAIA wa Nigeria, Okwubili Agu (40), amekamatwa katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA) akiwa na pipi 71 za dawa za kulevya
aina ya heroin, zenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 54, alizokuwa
amezimeza tumboni.
Kamanda wa Polisi wa Kikosi Maalum cha Kupambana na Kuzuia Dawa za
Kulevya nchini, Godfrey Nzowa alisema jana kuwa mtuhumiwa huyo
alikamatwa juzi majira ya saa 4 usiku katika uwanja huo. Nzowa alisema
kuwa mtuhumiwa huyo
alikamatwa na Kikosi Kazi kinachofanya kazi katika Uwanja huo, akiwa
katika harakati za kusafiri na ndege ya KLM kwenda Amsterdam, Uholanzi.
Credit:HabariLeo
Credit:HabariLeo
No comments:
Post a Comment