Jumuiya ya Watanzania wanaoishi nchini Oman (Tanzania Club in Oman-TANCO) ilifanya mkutano wake mkuu hapo Ijumaa tarehe 17.01.2014 mkutano uliohudhuriwa na watanzania jumla ya 150 wanaoishi na kufanya kazi nchini Oman.
Katika Mkutano huo Mwenyekiti wa TANCO ndugu Hassan Wazeer Mtonga alitumia mkusanyiko huo kutafuta usahihi wa habari zilizoenea pamoja na picha zikionyesha wanawake wawili wakiwa wameungua na kudai kuwa ni wadada Kakitanzania na kuwa wamefanyiwa ukatili huu na mabosi wao wa Oman.
Ndugu mtonga alieleza kuwa alizipata taarifa hizo na yeye kwa nafasi yake ya Uenyekiti aliziwasilisha Ubalozi wa Tanzania nchini Oman ambao nao walizifanyia kazi kushirikiana na Serikali ya Oman kupitia polisi, hospital na viwanja vya ndege, lakini taarifa hazikuonesha kuwepo kwa tukio hilo na kuthibitisha kuwa ni uzushi na uongo kwani hawakuweza kupata majina ya watanzania hao, waajiri wao na mazingira ya mashambulio hayo.
Ndugu Mtonga aliwaomba Watanzania wote waliohudhuria Mkutano huo ambaye anataarifa sahihi kuhusu matukio hayo aziwasilishe , lakini hakuna hata mmoja aliekiri kuwa na taarifa kamili zaidi ya kupokea picha hizo kupitia mtandao wa Whatsapp.
Mwenyekiti alisisitiza kuwa habari ile si ya kweli na kwamba ni uzushi usio na misingi yeyote ambao unaweza kuwa na athari kubwa katika mahusiano ya nchi.
Mwenyekiti alieleza kuwa habari hii ya uvumi wa kuunguzwa na kumwagiwa tindikali kwa watanzania haikupokelewa vizuri na wenyeji wetu wa Oman na kuwa inatishia kuharibu uhusiano wa kindugu na kihistoria uliopo baina ya Tanzania na Oman na pia watanzania na waoman kwa kupelekea kuzuiwa kwa watanzania kuja Oman kufanya kazi na hivyo kushindwa kutumia fursa za ajira zinazopatikana Oman.
Mwenyekiti aliwaasa watanzania kuwa makini na matumizi ya mitandao na kuepusha kutumia mitandao kusambaza habari ambazo si za kweli. Aliwaomba kuwa habari yeyote inayomuhusu mtanzania mahala pa kuanzia ni ubalozini au kwenye Jumuiya ya Watanzania nchini Oman.
Mwenyekiti pia aliwasihi wa Tanzania kufanya kazi kwa juhudi, maarifa na nidhamu ili kuijengea sifa nzuri Tanzania.
Aliwakumbusha Usia wa Rais Jakaya Kikwete alipokutana na watanzania wanaoishi Oman wakati alipotembelea Oman mwaka 2012 alipowausia watanzania kuwa raia wema na kujiepusha na vitendo vya uvunjaji sheria za nchi wanamoishi.
Aliwakumbusha Usia wa Rais Jakaya Kikwete alipokutana na watanzania wanaoishi Oman wakati alipotembelea Oman mwaka 2012 alipowausia watanzania kuwa raia wema na kujiepusha na vitendo vya uvunjaji sheria za nchi wanamoishi.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya watanzania Oman Ndugu Hassan Mtonga( Aliesimama) akiongea na Watanzania katika mkutano mkuu wa Jumuiya watanzania nchini Oman uliofanyika Muscat, Oman Ijumaa tarehe 17 Januari 2014.
Sehemu ya Watanzania wanaoishi nchini Oman wakiwa kwenye mkutano huo.
No comments:
Post a Comment