Sunday, 19 January 2014

MTANZANIA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 4 JELA BAADA YA KUKAMATWA NA MADAWA LA KULEVYWA NCHINI MAREKANI.

Mtanzania aliyekamatwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dulles uliopo Sterling, Virginia na madawa ya kulevya yenye uzito wa paundi 4 amehukumiwa kifungo cha miaka 4 jela baada ya kukubali kosa tarehe 26 April mwaka jana
Mtanzania huyo Omar Mohammed Omar mwenye umri wa miaka 40  alipatikana na madawa hayo alipojaribu kuyaingiza nchini Marekani kupitia uwanja huo wa kimataifa wa Dulles mwezi Octoba mwaka 2012. Alipopekuliwa na afisa wa Customs baada ya Omar Mohammed Omar kuwasili na ndege  akitokea Umangani, alipopekuliwa begi la mkononi alilobeba alikutwa na vipaketi vinne vyenye madawa ya kulevya ya aina ya Heoin yenye thaman ya dola za Kimarekani 225,000 kwa bei mtaani iliyokadiriwa na mahakama.
Tangia Octoba 1, 2011  mpaka Sept 30, 2012 uwanja wa ndege  Dulles imeishakamata watu 16 wa madawa ya kulevya yenye uzito wa paundi 61
Baada ya kutumikia kifungo Omar atarudishwa Tanzania na hataruhusiwa kuingia tena Marekani.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...