Mbunge wa Arusha, Godbless Lema,
ameendelea kushikilia madai yake kuwa polisi wanahusika na tukio la bomu
lililolipuka katika mkutano wa kampeni ya chama hicho Viwanja vya
Soweto Arusha na kusababisha vifo vya watu wanne.
Lema alitoa madai hayo juzi alipohutubia mkutano wahadhara Viwanja vya Shule ya Msingi Ngarenaro.
Alidai Rais Jakaya Kikwete amegoma kuunda tume huru ya kimahakama kuchunguza tukio hilo, ili kunusuru polisi na aibu ya kushiriki uhalifu na mauaji ya raia wasio na hatia.
“Mauaji ya Soweto yalipangwa na kutekelezwa na polisi, RPC (Kamanda wa Polisi) wa Arusha anajua mpango mzima ndiyo maana Rais hataki kuunda tume kama Chadema tulivyomuomba, ili tuwasilishe ushahidi wa video kuonyesha jinsi walivyohusika,” alisema Lema

No comments:
Post a Comment