Wednesday, 24 July 2013

HAKUNA UBISHI WANAUME WENGI HUPENDA KUTOKA NJE YA NDOA

Uvaaji wa wanawake wa namna hii huamsha hamu ya tendo la ndoa kwa mwanaume kwa kiwango kikubwa sana....

Carol Botwin ambaye ni mtaalamu anayeaminika sana kwenye masuala ya tendo la ndoa na uhusiano akiwa ameandika vitabu kadhaa kuhusu mambo hayo, kama kile cha Men Who Can’t Be Faithful, anasema, wanaume kutoka nje, siyo jambo wanalopanga, bali hujikuta tu na kujilaumu au kushangaa baadaye.
CONTINUE READING
Imekuwa ikisemwa kwa siku nyingi na wataalamu wengi kwamba, wanaume hawahusishi kupenda na tendo la ndoa. Nadharia hii inaonekana kushika mizizi baada ya wengi kukubaliana nayo kufuatia utafiti wa kina kuhusu tabia za wanaume na wanawake katika mapenzi.

Kuna mifano mingi yenye kuashiria kwamba, huenda kuna wanaume wachache sana kama mimi ambao hawatoki nje, tena wachache sana. Hii inatokana na ukweli kwamba, hamu au msukumu wa wanaume kutoka nje ni kama wa kimaumbile, umejengwa ndani ya mwanaume, haupo nje.

Mwanaume anapotoka nje ya ndoa, hatoki kwa sababau anataka sana kutoka, hutoka zaidi kwa sababu kuna msukumo wa kutoka. Hatoki nje kwa sababu anampenda huyo anayetoka naye nje, hapana. Anatoka nje kwa sbabau anasukumwa na asichokijua.

Kwa hiyo wanawake wana changamoto kuhakikisha kwamba, wakati mwingine wasione aibu kuwalinda waume au wapenzi wao, kwani linapokuja suala la kutamani na kutenda, wanaume zao ni sawa na Beberu la mbuzi. Hadi wamalize au kukamilisha kiu yao, ndipo akili zao za kibinadamu zinaporejea.
Ndiyo maana hata mwanamke anashauriwa anapomfumania mumewe ajiulize kuhusu kiwango, namna ilivyotokea na kwa nini. Kama ni mara ya kwanza anamfumania, kama siyo kwa rafiki wa mke au mwanamke ambaye anawagusa wote wawili moja kwa moja na kama ilikuwa wanajificha sana na kufanya siri kubwa, mwanamke anatakiwa ajue kwamba, huenda mume amesukumwa na yale maumbile niliyozungumzia.

Kwa nini mwanaume anatoka nje na anafumaniwa, anaomba radhi, anasamehewa na halafu anatoka tena nje. Mke akitaka kuondoka, anatumia kila gharama kumzuia. Kama hampendi anamzuia wa kazi gani? Kama ingekuwa kutoka nje ni sawa na kupenda kwa mwanaume, si angeachana na mkewe na kubaki na huyo hawara?

Ni kweli kwamba, baadhi ya wanaume hutoka nje kwa sababau wamewachoka wake zao, lakini wengi hutoka nje kwa kusukumwa na mauambile tu. Mwanaume huvutwa na mwili tu wa mwanamke, siyo kitu kingine. Kwa namna anavyovaa tu, mwanamke huweza kumvuta mwanaume kwa kiwango cha juu sana. Nikisema kumvuta nina maana ya kumtamanisha.

Wataalamu wengi wanasema nguo zenye kuchokoza kama vile zile za kubana au nusu uchi kwa ujumla, huamsha hamu ya tendo la ndoa kwa mwanaume kwa kiwango kikubwa zaidi, kuliko mwili wa kike ulio uchi.

Kwa hiyo wanawake wana changamoto kuhakikisha kwamba, wakati mwingine wasione aibu kuwalinda waume au wapenzi wao, kwani linapokuja suala la kutamani na kutenda, wanaume zao ni sawa na Beberu la mbuzi. Hadi wamalize au kukamilisha kiu yao, ndipo akili zao za kibinadamu zinaporejea

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...