Msanii chipukizi wa Bongo Muvi nchini Gado Balotel akiwa mwenye huzuni baada ya kuvunjika kiuno na miguu yote.
Hapa kama inavyoonekanamiguu ya Gado Balotel na bandeji baada ya kuvunjika yote mara baada ya kujirusha toka ghorofa ya 5 CONTINUE READING
Mshare unamuonesha Gado Balotel akiwa kwenye kava la moja ya filamu zake alizocheka kabla ya kukumbwa na balaa hilo.
Msanii na Kiongozi wa kundi la Bongo
Muvi nchini JB ambae ameombwa na wasanii kuchangisha harambee haraka ili
kupata fedha za kumsadia msanii mwenzao huyo anaeishi kwa mateso
makali.
Msanii na mwanamasumbwi wa zamani Fike
Wilson ambae amepongezwa na wadau baada ya kujitolea kumsaidia msanii
huyo, ambapo kwa sasa anaishi nyumbani kwa Fike huku akiwa anabebwa
kupelekwa chooni na kurudishwa pia.
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania
Saimon Mwakifwamba nae pia ameombwa kuungana kwa pamoja na wasanii
wengine kumsaidia msanii mwenzao anaishi kwa mateso makubwa usiku na
mchana.
Na Livingstone Mkoi
Msanii
nyota toka kiwanda cha muvi za kibongo nchini Maulidi Mfaume maarufu
kwa jina la Gado Balotel sasa amekumbwa na balaa la aina yake baada ya
kuvunjika miguu yote miwili pamoja na nyonga kuteguka baada ya kudondoka
toka ghorofa ya nne alipokuwa akiigiza filamu ya msanii mwingine aitwae
Baga.
Baada
Xdeejayz na kituo cha luninga cha DTV kupata taarifa hizo lilipiga
hatua ndefu hadi mahala anapojiuguzia msanii huyo ambako ni nyumbani kwa
msanii Wilson Fike maeneo ya Home Alone Vijana Kinondoni na kuonana uso
kwa uso na msanii huyo aneishi kwenye maumivu makali.
Akiongea
na mwandishi wetu nyumbani hapo Balotel alisema alikutwa na balaa hiyo
wiki mbili zilizopita akiwa Location ndani ya hotel ya Con Way iliyopo
Magomen Kagerana wasanii wenzake kama Hemed, Baga, Manaiki Sanga na
wengineo wakati wakiigiza.
Balotel
aliendelea kusema kuwa wakati shughuri za kuigiza ziliendelea na kuna
sini moja iliyokuwa inahitajika kuigizwa kwa mfano ikimtaka mtu aigize
kama anataka kujirusha kwenye ghorofa lakini asiruke ili kameraman kuchukua picha achukue shoti hiyo kisha mtu huyo aende chini kisha achukuliwe shoti nyingine ya kujifanya ametua chini.
Msanii
huyo aliendelea kusema kuwa nafasi hiyo ilibidi aigize msanii mwenye
filamu Baga lakini kutokana na uwoga wa msanii huyo alikuwa akijishauri
namna ya kuigiza kuruka ghorofani ndipo Ballotel akamtoa pembeni na
kumuonesha namna ya kuruka kama Jet Lee huku akimwambie mwenzake hiyo
ilikuwa kazi ndogo sana.
Msanii
huyo aliendelea kusema kuwa baada ya hapo alijikuta ameruka toka
ghorofa ya nne, lakini aliendelea kusema“ Wakati nikiwa bado sijashuka
chini njiani nilianza kuhisi harufu ya kifo kwani tayari nimuona Israel
mtoa roho akinipungia mkono na hatimae nilitua chini kwa kufikia miguu” Alisema Ballotel
Hata
hivyo kijana huyo aliongeza kusema kuwa mala baada ya kutua nchini
alihisi moto unawake miguuni mwake huku harufu ya damu ikimtoka puani na
mdomoni na baada ya kujiangalia aliona visigino vyake vikiwa vimepasuka
vyote huku tumboni kukiwa na maumivu makali sana kumbe wakati huo
nyonga ilikuwa imeachia huku miguu yake ikiwa imesogea tumboni.
Gado
alisema baada ya tukio hilo wasanii wenzake walimchukua na kukmimbiza
Hospital ya Mwananyamala mbapo dakika chache baadae walimkimbiza
Muhimbili kwa matibabu zaidi.Msanii huyo ambae ametamba sana kwenye
filamu kama Going Bongo,Msitu wa Hifadhi,Tumbo Joto na Escap ambayo
alikuwa akiigiza siku ya tukio lililomkuta.
Aidha
msanii huyo aliendelea kusema kwa sasa anaishi kwenye mateso makali
huku wasanii wenzake wakishindwa kumpa ushirikiana “Hapa nilipo nalelewa
na Fike Wilsoni ndiye anaenibeba kwenda chooni na kunirudisha kwa kweli
hali yangu sio nzuri nahitaji msaada wa wasanii wenzengu, Wako
wanaokuja kunirushia chochote kama
Kalapina,Young
Killer na madaktari wanasema huenda wakanishauri kwenda India ili
wakazirekebishe nyonga zangu” Alisema Gado na kuongeza kuwa anawaomba
wasanii wenzake wasamalia wema kumsaidia kwani hali yake ni mbaya na
huenda kwa mujibu wa madakatari wake akahitajika kupelekwa India ili
kukinusuru kiuno chake la sivyo hatozaa tena kwa vile nyonga
vimeshafyatuka.
No comments:
Post a Comment