Uvumi wa ziara ya Obama kuvunjika nchini Tanzania ulienea Ijumaa kwenye radio mbao na watu mbali mbali nchini Kenya na Tanzania.
Uvumi huo pengine umetokana na watu kutokuelewa au kukanganywa na taarifa ya gazeti la Washington Post hapa Marekani au baadhi tu ya watu kuamua kutoa maneno hayo.
Lakini ukweli unabaki kwamba Obama anakwenda Tanzania kama ilivyopangwa ila kuna mabadiliko katika mpangilio wa ziara hiyo.
Mabadiliko hayo kwa mujibu wa vyombo vya habari ni kwamba Obama hatakwenda kwenye mbuga za wanyama nchini Tanzania badala yake atatumia muda huo kwenda Afrika Kusini katika kisiwa cha Robin Island.
Gazeti la Politico lilitoa lawama kwa gazeti la Washington Post kwa kuripoti kubadilishwa kwa safari hiyo bila kukiri kwamba sivyo walivyoripoti awali na kueleza kana kwamba hayo hayakuwa mabadiliko yoyote. Kwa taarifa hiyo bofya hapa.
http://www.politico.com/blogs/media/2013/06/washington-post-changes-story-about-obama-africa-trip-166267.html
Wakati huo huo gazeti la Washington Post limekuwa likihoji ziara ya Obama nchini Tanzania ikiwa nchi hiyo inadaiwa kukiuka haki za binadamu na wakjati huo huo wakihoji juu ya matumizi ya serikali ya Obama inayokadiriwa kuwa kati ya dola milioni 60 hadi 100.
Katioka moja ya makala ya waandihi wa Washington Post mwandishi Dan Millibank anahojki ziara ya Obama nchinin Tanzania ikiwa nchi hiyo inashiriki kukiuka haki za binadamu kutokana na kesi ya mmoja wa maafisa wake wa ubalozi wa zamani hapa Washington Dc. Bofya hapa kwa makala hayo.
http://www.washingtonpost.com/opinions/dana-milbank-obamas-ill-advised-visit-to-tanzania/2013/06/07/397b00fa-cf88-11e2-8845-d970ccb04497_story.html
No comments:
Post a Comment