Friday, 28 June 2013

UPDATE KUTOKA DODOMA: SUGU ASHINDA KESI BAADA YA KUMTUKANA WAZIRI MKUU:

Leo asubuhi Joseph Mbilinyi (Sugu) alipelekwa mahakamani kwa shitaka la kutumia lugha ya matusi dhidi ya Waziri Mkuu, shtaka hili lilifunguliwa kwenye mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Dodoma na mwendesha mashitaka wa serikali.

Baada ya kufunguliwa shtaka hilo, Lissu ambaye alikuwa wakili wa Sugu aliitaka mahakama ifutilie mbali shtaka hilo kwani halina msingi wowote wa kisheria na baada ya mabishano ya kisheria baina ya Lissu na wanasheria wa serikali kushindwa kuthibitisha kuwa neno Mpumbavu ni lugha ya matusi, hakimu ameamua kufuta shtaka hilo na ametangaza kuwa Sugu yuko huru na hana kesi ya kujibu.
 

Muda huu ndio wanaondoka mahakamani, Sugu, Lissu na baadhi ya wabunge na viongozi wa CHADEMA ambao walikuwa mahakamani hapo.
 

My take: 

Polisi na serikali, mnaendelea kujidhalilisha kwa kufungua kesi ambazo zinaendelea kuwavunjia heshima mbele ya mahakaama na umma wa wa tz. Acheni kufuata maelekezo ya kina Mwigulu, hawajui sheria, hawajui misingi ya kufungua kesi, nyie kila siku mtakuwa mnafungua kesi mpaka lini wakati mnashindwa kila leo?

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...