Wednesday, 12 June 2013

OFISI YA MAKAMU WA RAIS KUPITIA TAASISI YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA, YAKABIDHI MSAADA WA KOMPYUTA KWA KITUO CHA MAFUNZO YA KOMPYUTA CHA CHWAKA MJINI UNGUJA

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Dkt. Idrisa Muslih Haji (kulia) akikabidhi sehemu ya Compyuta 15, kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya jimbo la Chwaha Bw. Muhammed Ali Selemani, ikiwa ni sehemu ya ahadi ya Mhe. Makamu, kwa Kituo hicho cha Chwaka Computer Training Center. Makabidhiano hayo yalifanyika jana Juni 11, 2013, kwenye Kituo hicho. Kulia ni Mtendaji Mkuu Ofisi ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Bw. George Mulamula.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Maendeleo ya jimbo la chwaka wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Kusini Uguja, (hayupo pichanio) wakati alipokua akizungumza baada ya makabidhiano hayo, alipomwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Dkt. Bilal.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Dkt. Idrisa Muslih Haji (kulia) akikabidhiwa sehemu ya Compyuta 15, na Mtendaji Mkuu Ofisi ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Bw. George Mulamula, ambapo Mkuu huyo wa mkoa wa Kusini unguja, alizikabidhi kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya jimbo la Chwaha Bw. Muhammed Ali Selemani, kwa niaba ya Mhe. Makamu wa Rais Dkt. Bilal, kwa ajili ya Kituo cha Chwaka Compyuter Training Center, ikiwa ni sehemu ya ahadi ya Mhe. Makamu Dkt. Bilal kwa kituo hicho. Makabidhiano hayo yalifanyika jana Juni 11, 2013, kwenye Kituo hicho. Kulia ni . Kushoto ni Naibu Katibu wa Makamu wa Rais, Mohamed Khamis.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Dkt. Idrisa Muslih Haji, akizungumza na Wajumbe wa kamati ya Maendeleo ya Jimbo la Chwaka mara baada ya makabidhiano ya Computer 15, ikiwa ni sehemu ya ahadi ya Makamu wa Rais Kwenye Kituo cha Chwaka Computer Training Center. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Chwaka Bw. Muhammed Ali (kushoto) ni Shekha wa Shehia ya Chwaka Bw. Msaraka Pinja na Mtendaji Mkuu wa Sayansi na Teknolojia Bw George Mulamula. Makabidhiano hayo yalifanyika jana Juni 11, 2013, kituoni hapo. Picha na OMR.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...