Tuesday 11 June 2013

HIKI NDO SABABU ALIYOITOA 2O PERCENT, KUHUSU KUTOONEKANA KABISA KATIKA MSIBA WA NGWAIR

 
Mwnamuziki aliyewahi kuvunja rekodi ya mwaka 2010 kwa kunyakua tuzo tano kwa mfululizo Abasi Kizasa" 20 pacent" ameibuka na kutoa sababu za msingi za kushindwa kwenda kushiriki kwenye mazishi ya mwanamuziki mwenzake Arbeth Mangwair kutokana na kuuguliwa sana babaake mzazi ambae ana kansa ya utumbo.
Akiongea na Xdeejayaz 20 pacent alisema kuwa " Siku wakati watu wanaondoka kwenda Morogoro kuzika huku mimi babaangu alikuwa hali mbaya sana na alikuwa amelazwa Hospitalini hiyvo isingekuwa rahisi kumuacha akiwa kwenye hali ile na mimi ndo nilikuwa msimamizi wa kila kitu" Alisema mwanamuziki huyo.
Hata hivyo mwanamuziki huyo alimaliza kusema kuwa kifo cha mwangwair ni pigo kubwa sana kwake kwa vile walikuwa wanashirikiana mambo mengi sana kuhusu muziki na kujipanga namna kukabiliana na maharamia wa muziki wanaotaka kuamudiwa kama Mungu ili nyimbo zao zipigwe. Lakini licha ya hayo yote Mungu kampenda zaidi Jina lake rihimidiwe Milele Amina.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...