Baada ya watu wengi kuzipata habari na bila kujua imekuaje kwa Mtanzania anaedaiwa kukamatwa na dawa za kulevya nchini Egypt na kwamba alikua anakaribia kunyongwa, balozi Mohamed Haji wa Tanzania nchini Egypt ameongea Exclusive na millardayo.com na kueleza yote anayoyafahamu kuhusu hii ishu. Namkariri akizungumza 1. Ni kweli kuna raia wawili Watanzania wamekamatwa na dawa za kulevya ambao ni Mbarak Abdallah Salim (28) na Sharifa Mahmud (27) wakazi wa Magomeni Kagera Dar es salaam, wanaundugu wa mtoto wa shangazi na mjomba. 2. Walikamatwa tarehe 16 May 2013 wakati wakiingia Misri, kwa mujibu wa maelezo safari yao ilianzia Dar es salaam kwenda Mombasa, Nairobi mpaka Misri. |
4. May 18 2013 ndio tuliitwa kwenda kutazama Raia wetu, nikatuma maafisa wawili wazuri kwenda kutazama ili raia wetu wasimbambikiwe kesi.
5. Baada ya hapo waliwekwa rumande na tukapata nafasi ya kuwaunganisha na nyumbani huku Tanzania wakaongea kwenye simu kilichowapata.
6. 26 May 2013 ndio walipelekwa Mahakamani kwa mara ya kwanza na kurudishwa rumande wote wawili.
7. Hawa ndio Watanzania wa kwanza kukamatwa na kesi kama hii na ikithibitishwa wamefanya kweli, hili kosa ndilo litakua doa la kwanza kwa Tanzania hapa Misri.
8. Ishu ya kunyongwa, tunajaribu kufanyia kazi lakini hakuna kumbukumbu za mgeni yeyote kwa sisi tunavyojua ambae amewahi kunyongwa kuhusu ishu ya dawa za kulevya.
9. Tunajitahidi kuwasiliana na mamlaka zinazohusika ili kujua siku gani watapelekwa tena Mahakamani alafu tutawafahamisha nyumbani.
Kwa ushahidi unaweza kumsikiliza balozi hapa chini na pia kutazama video hapo chini ya ushahidi wa kukamatwa na dawa za kulevya…
No comments:
Post a Comment