HAMMER Q AFUNGUKA YA MOYONI KUHUSIANA NA MAPRESENTER WAPENDA HELA NA KUHUSU WASANII KUTHAMINIKA WAKISHAKUFA. SOMA HAPA ALICHOKISEMA
wasanii tunafanya kazi ili tupate maslahi na tufaidi matunda ya mziki kabla hatujakata roho kabla hatujafumba macho lkn hakuna kitu km hicho kwa sasa mziki wa bongo bila ya kuhonga pesa umekuwa mgumu na km ukitaka promo ya bure inabidi usubirie siku ukifa , ninajitahidi kufanya kazi mpya na kupeleka radio lkn haziskikii kuna baadhi ya watangazaji hupiga kzi kwa moyo mmoja kwa kujua uwezo wangu wa kazi (big up kwao) wengine nahisi watakuwa wanazihifadhi chumba maalum mpaka siku nitakapokata roho ndo zitaskika kila sekunde na hata mtangazaji ambae hajawahi kutaja hata jina langu basi siku hiyo ataniandalia kipindi maalum kitakachonizungumzia mimi,, na kazi zangu zitaskika mpaka zilizokuwa hazijawahi kuskika kiukweli baadhi ya watangazaji hamtufanyii pw wasanii, mfano jana nimesambaza nyimbo mpya niliofanya na wife wangu lkn cha kuniskitisha unaenda sehem mtu anakudai hela live hajiulizi kichwani mara mbili kwamba huyu kijana mwenzangu na hii ndo kazi yake bila ya kuipiga hawezi pata hela au munahisi tunakisima cha hela?? ,unajisahau kuwa ww unamshara hapo kazini lkn mimi sina mshara kama hujapiga kazi yangu, hiki kilio sio changu peke yangu wengi wanalia mpaka wengine wanaamua kukimbia nchi,wengine wanakua pusha inafika wakati tuhurumiane km binaadam,nimesoma kupitia misiba ya wasanii wenzangu kwamba ukikata roho unapata promo ambayo ulipokuwa hai hukuipata nimeona nije na mbinu m,badala , mbinu ambayo itafanikishwa na mashabiki wangu na marafiki zangu na kila mtu anaependa kazi zangu,;;,, mda wowote , siku yeyote , sekunde yeyote nikikata roho mwenyezimungu atakapochukua uhai wake basi dj yyt ambae unaona alikuwa hapigi kazi zangu nilipokuwa hai basi mfateni huyo dj na alipie laki mbili hapo hapo kwa kila atakapopiga kazi yangu na akiniandalia kipindi maalum alipie milioni moja, zoezi hili liwe kwa mda wote wa maombolezi yangu , na hela itakayopatikana hapo igawanywe mara mbili nusu iende kwa familia yangu na nusu ipelekwe ktk vituo vya kulelea watoto yatima 7bu nina malengo ya siku nyingi kuanzisha kituo cha kulelea watoto yatima ,lkn hayajatimia 7bu kazi haiendi vizuri ,, inafika hatua siku hizi tunasambaza kazi zetu kwa madereva boda boda na wanaochoma cd na kutumiana whatsapp na bbm ila baadhi ya radio mpaka uwe na mtu(kujuana) au mkwanja kwenye meza, nilishawahi kwenda radio moja nikaambiwa ili kazi yangu isimame niweke milioni kwenye meza kisha shuguli yote niwaachie wao hapo wananambia hivyo najua ,wenyewe mfukoni nipoje kwanza asubuhi yenyewe nimekopa mihogo miwili kwa mama miki anadai mia mbili na kufika hapo radio nilipata lifti kwa swaiba wangu @amoc b hokororo na msosi wa mchana sijaujuwa bado ,unafkiri milioni moja ntaitowa wapi basi waliponambia hivyo nikarudi na kazi yangu nyumbani kilichobaki nawatumia masela wangu kwenye whatsapp tu mpaka ss nimeamua sifanyi mziki kimaslahi cos hakuna sasa hivi nafanya mziki 7bu naupenda na nina albam 3 naskiliza maskani na masela wangu **jali kazi yangu nikiwa bado nipo hai
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment