ALIYESEMA dunia ni hadaa, ulimwengu shujaa hakukosea. Msichana mmoja ambaye alikuwa akifanya kazi za ndani (hausigeli), Devotha Sanga (18), amejinyonga baada ya kushindwa kuelewana na mpenzi wake.
Hiyo ni barua alomwandikia mpenzi wake.
“Aliponituma dukani nilimuacha akiandika barua ambayo ilikutwa na polisi baada ya kujinyonga,” alisema Hellen.Hata hivyo, Hellen alisema baada ya kufika dukani aliambiwa hakuna simu ndipo alipoamua kurudi nyumbani lakini cha kushangaza alikuta milango yote imefungwa, akaanza kugonga huku akimwita Devotha bila mafanikio.
Majirani waliokuwa eneo hilo walisogea kwa lengo la kumsaidia mtoto huyo lakini pia waligonga mlango bila kupata majibu ndipo walipoamua kuvunja na kuingia, wakamkuta Devotha ananing’inia akiwa amejinyonga kwa kutumia shuka.
Polisi kutoka Kituo cha Sitakishari walifika eneo la tukio na kuufanyia uchunguzi mwili kisha kuchukua pamoja na barua na simu yake ambayo muda mfupi kabla ya kifo chake ndiyo aliyokuwa akiitumia kuwasiliana na mpenzi wake aliyejulikana kwa jina moja la Christopher.
Naye kijana mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Peter ambaye ni muuza duka karibu na nyumba hiyo, alisema siku ya tukio Devotha alikuwa hana raha na kila mara alikuwa anakimbiakimbia kama mtu aliyechanganyikiwa.
Mwajiri wa Devotha, anayejuikana kama Mama Hellen Patrick ambaye ni askari, alisema msichana huyo alikuwa mchapa kazi na mwaminifu sana.
Mwili wa Devotha uliagwa Juni 7, mwaka huu katika Hospitali ya Muhimbili na kusafirishwa kupelekwa wilayani Makete, Njombe kwa mazishi.
No comments:
Post a Comment