Mambo yaliyomfanya Mbunge wa arusha
Godbless Lema akamatwe na kunyimwa dhamana jioni hii ni haya yafuatayo
baada ya kuongea na Mwanasheria wa Lema wakili Humphrey Mtui
i)Kosa la kwanza ni kuwaambia
wanafunzi wa chuo cha uhasibu alipoenda kuwatuliza kuwa ‘dhambi kubwa
kuliko zote ni woga ‘.Haki hutafutwa na kupiganiwa ikiwa jambo
unalipigania ni la msingi na linafaa kupiganiwa(Worth fighting for)
ii)Kosa la pili ni pale alipotamka
kuwa ‘’Tumemtafuta mkuu wa mkoa juu ya Matatizo yenu na mlivyoshuhudia
hapa amechukua muda mrefu na kuingia kama vile anaingia kwenye
send-off.Hawa ndiyo viongozi wetu ambao hawajali matatizo ya
wananchi’’Kwa hiyo huo ni uchochezi
iii)Kosa la Tatu ni pale
alipotamka kuwaambia wanafunzi kuwa ‘’Mimi Mbunge wenu nipo sambamba
nanyi hadi mpate haki yenu na ikiwa mkuu wa mkoa hatakuja hapa kama
mwenyekiti wa kamati ya ulinzi wa mkoa nitawaongoza hadi ofisini kwake
ili mpate majibu na haki yenu kwani ni haki yenu ya msingi kwa mujibu wa
katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ambayo niliapa kuilinda
Bungeni na pia inaruhusiwa kwa mujibu wa kikanuni na kifalsafa katika
utekelezaji wa utawala bora wa kidemokrasia ambao msingi wake ni
kusikilizwa na kulinda haki za binadamu’’Huu nao umeitwa kwamba ni
uchochezi.
Sasa haya maneno hapo juu ndiyo
yaliyosababisha jeshi la polisi kuvamia nyumbani kwake usiku wa manane
na kuzua taharuki maeneo hayo na ndani ya nyumba yenye ndugu jamaa na
hata mtoto mwenye miezi mitano huku polisi wakitumia nguvu na kukiuka
sheria
Huo umeitwa uchochezi baada ya
mkuu wa mkoa kumtumia ujumbe wa mkononi kupitia simu yake kupitia namba
0752960276 aliyotishia kumbambikizia kesi anayoitaka yeye.
Sasa hayo waliyoita makosa ya uchochezi ndiyo yaliyomnyima haki ya dhamana leo.tutafakari kama Arusha itatawalika kwa hali hii.
Hebu tupime makosa hayo matatu kama yanaweza ku-justfy mambo yote yaliyotokea.
No comments:
Post a Comment