Wednesday, 1 May 2013
BEYONCE AWAPIGA MKWARA WAPIGA PICHA, HIKI NDO ALICHOKISEMA
Baada ya kukerwa na picha alizopigwa wakati wa tamasha la SuperBowl ambazo anaona zilimdhalilisha, mwanamuziki Beyonce amefikia maamuzi magumu ya kuwakataa wapiga picha
Kwa mujibu wa barua pepe iliyotumwa kwenye ukurasa wa facebook wa Umoja wa Wapiga picha za Muziki imeeleza kuwa mwanamuziki huyo haitaji tena wapiga picha katika shoo za ziara yake ya sasa ya Ulaya
Badala yake amekuwa akitoa picha rasmi zilizopigwa kutoka katika shoo na wapiga picha maalum aliowakodisha
Labels:
majuu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment