Nina mpenzi wangu anayefanya kazi Morogoro, mwezi march alikuja 
kunitembelea sababu alikuwa likizo na alikaa kwangu wiki 2 na siku 3 
tangu afike. Alishikwa na malaria kali ikabidi niombe ruhusa kazini ili 
nimuuguze.
Kiukweli nilimpa kila kitu anachotakiwa kupewa mgonjwa including 
dawa,vyakula vilivyopendekezwa na daktari na vyakula alivyopenda 
mgonjwa, pamoja na gari kumpeleka hospitali au sehemu yoyote aliyopenda 
ili kumliwaza mgonjwa. Mungu akasaidia akapona na amerudi morogoro.
Lakini cha ajabu juzi ananiambia sikumjali alipokuwa anaumwa sababu 
sikuwahi kumletea kadi ya get well soon pamoja na Mauwa kama wenzake 
wakiumwa wanavyofanyiwa. Ebu nisaidieni kadi na maua tu ndio mtu 
akujali?


No comments:
Post a Comment