Thursday 23 January 2014

UNAAMBIWA BONGO MOVIE NI MAJANGA MATUPU...HUYU HAPA RICHIE ANAKIRI KUFANYA MADUDU WAKATI AKIWA KIONGOZI...!

MKONGWE katika anga la filamu za Kibongo, Single Mtambalike ‘Richie’ amekiri kutumia vibaya madaraka wakati wa uongozi wake kama mweka hazina wa Klabu ya Bongo Movie msimu uliopita. 
 
Single Mtambalike ‘Richie’.
Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar, Richie alisema kulikuwa na mfumo mbovu wa jinsi ya kutumia pesa.
“Kuna mazuri tulifanya pia mabaya yapo hususan mfumo mbovu wa jinsi ya kutumia pesa, kiongozi yeyote aliweza kuchukua pesa bila kuhojiwa na hata mimi nilikuwa natumia vibaya,” alisema Richie.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...