Saturday 25 January 2014

"NAHITAJI SIKU NIKIWA NAJIFUNGUA LEBA MUME WANGU AWEPO PEMBENI AKIANGALIA JINACHOENDELEA" IRENE PAUL

Mcheza filamu  anayeng’ara katika tasnia ya filamu Bongo Irene Paul ametoa kali ya mwaka baada ya kudai kuwa hivi karibuni anatarajia kubeba ujauzito na kujifungua lakini ikifika siku ya kujifungua lazima mumewe awe pembeni yake akishuhudia akijifungua, hiyo kwake itakuwa ni sehemu ya faraja na kumuonyesha ni jinsi gani wanawake wanatakiwa kuheshimiwa kwa kuwaletea watoto wanaume. 
Nimepanga nitapoamua kuzaa tu lazima siku ya kujifungua Mr. yaani mumewe wangu awe pembeni akishuhudia kazi ya kuzaa ilivyo na shuruba maana mtu mwingine unakuta inafikia muda anakuwa hana mapenzi na mke wala watoto nina imani akiniona ninavyotabika hatanisumbua wala kukosa mapenzi na mimi, kama nilivyosema na itakuwa hivyo,”anasema Irene Paul.

Amezidi kusisitiza kuwa atafanya hivyo katika kujenga mapenzi ya dhati kwa mumewe kwani shida ambazo upata akinamama wakati wa uzazi wengine hata uapa kama hawatazaa tena lakini baada ya kujifungua upotea usahau na kuwa ni jambo la kawaida, Irene anasema anajua wengi watamshangaa lakini itakuwa kuingilia uhuru wake kwani hata Ulaya wasanii nyota na watu wengine ujifungua mbele za waume zao labda huku ni kukosekana kwa ujasiri kati ya wanaume na wanawake pia alimalizia mwanadada huyo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...