Na Imelda Mtema
NI mkasa wa kusikitisha kama siyo kutisha, unaowafanya wanaume wengi wa siku hizi waonekane ni makatili na majanga matupu mbele ya jamii.
Akizungumza na Joyce Kiria(kulia), Leah (kushoto) alisema kwamba siku zote aliishi na mumewe kwa uvumilivu mkubwa.
Kitendo hicho cha kinyama, kimemkuta mwanamke Leah Benard mkazi wa Kijiji cha Kifufu, mkoani wa Geita baada ya kukatwa kiganja chake cha mkono kwa panga na mumewe (jina kapuni).Kisa cha kufanyiwa unyama huo kinadaiwa kuwa ni mwanamke huyo kukataa kwenda kuchukua chakula kwa mama yake mzazi ili familia hiyo ile.
Mkono wa Leah baada ya kukatwa na mumewe.
Akizungumza na mwandishi wetu, Leah alisema kwamba siku zote aliishi na mumewe kwa uvumilivu mkubwa kutokana na vipigo vya mara kwa mara alivyokuwa akivipata.“Nilikuwa nikipokea vipigo vikali wakati mwingine bila sababu za msingi lakini nilikuwa nikivumilia.
“ Kisa cha kukatwa mkono ni kukataa kwenda nyumbani kwa mama yangu kuchukua chakula cha kula pale nyumbani, kitu ambacho ni kinyume na utaratibu wetu wa maisha,” alisema Leah.
Mwanamke huyo alisema kwamba mumewe alimlazimisha kwenda kuchukua chakula hicho lakini alipokataa alipigwa na kulazimika kuondoka mpaka nyumbani kwa wazazi wake kukwepa kipigo zaidi.
Leah aliendelea kudai kwamba siku nyingine saa saa mbili usiku akiwa anapika chakula cha familia, alishtukia mkono wake ukiwa umebaki mfupi na kusikia maumivu makali, alipogeuka akamuona mumewe akikimbia.
“Sikuwa na wazo lolote nilikuwa nikipiga kelele ya kuomba msaada na baadhi ya majirani wakajitokeza kwa kuwa damu zilinitoka kwa wingi nikapoteza fahamu,” alisema Leah.
Leah aliongeza kuwa alizinduka akiwa akiwa hospitali kitu ambacho kilimfanya ajisikie vibaya kwa kuwa hakuwa na kosa la kusababishiwa ulemavu wa ukubwani.
Mwenyekiti wa kitongoji hicho cha Kifufu, Ali Malima, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa kijiji kinamsaka mume wa Leah.
Kutokana na kitendo hicho alichofanyiwa, mwanamke huyo amelazimka kuwa na maisha magumu hivyo anawaomba Watanzania walioguswa na habari hii wamsaidie kumchangia ili aweze kupata mkono wa bandia.
Kama umeguswa na matatizo yake, unaweza kumchangia kwa namba 0753 787126.
Shukurani zaidi ziende kwa Wanaharakati wa Kutetea Haki za Wanawake (HAWA), Joyce Kiria kupitia kipindi chake cha Wanawake Live kwa kuweza kufutilia habari hii kwa kina.
No comments:
Post a Comment