Na Hamida Hassan
BONGO Muvi kimenuka! Viongozi wapya wa Klabu ya Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ (mwenyekiti) na William Mtitu (katibu), wametofautiana kauli na kuanza kurushiana maneno mazito wakitaka kukunjana mbele ya wajumbe wa klabu hiyo.
Chanzo makini kilitonya kuwa, kilichosababisha kuibuka kwa ugomvi huo ni baada ya Steve Nyerere kutoa wazo la filamu inayoitwa Baba Chodo yenye lengo la kuingizia fedha ndani ya klabu hiyo na kiasi kidogo kubaki kwake kama mwanzilishi wa wazo.
“Unajua Steve alikopa fedha sehemu Sh. milioni 10 na akasema kuwa mwenye fedha anataka turudishe milioni 15 hivyo baada ya kuuza filamu hiyo kwenye Kampuni ya Proin Promotion ambayo inatarajia kuwalipa Sh. milioni 50.
“Kule walikokopa watarudisha milioni 15, milioni 5 watawapa wasanii watakaocheza kisha milioni 10 atachukua Steve Nyerere aliyetoa wazo na milioni 20 itaingia kwenye mfuko wa Bongo Movie ndipo mtiti ulipoibuka, Mtitu hakiridhia, akahoji,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
“Mtitu alimchana laivu Steve Nyerere kuwa ni mwizi na aliwahi kuiba fedha za klabu kipindi cha nyuma kabla hajawa mwenyekiti wa klabu. Hapo ndipo moto ukawaka zaidi.”
Sosi huyo alieleza kuwa, walipoanza kukwidana, Mkurugenzi wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, Asha Baraka aliwakalisha chini kisha akawasema kwa kugombana mbele ya wanachama wao, Mtitu akaomba msamaha kwa bosi wake.
“Huwezi amini pamoja na Mtitu kuomba msamaha kwa Steve Nyerere, Steve alimwambia hawezi kukaa naye meza moja wakaelewana kwa sababu ni mtu ambaye haelewi na hamalizagi mabifu,” alisema sosi huyo.
Baada ya habari hizo kutua kwa paparazi wetu, alimpigia Steve Nyerere kumuuliza undani wa sakata hilo ambapo alisema kuwa yeye hana tatizo na mtu lengo lake ni kusaidia klabu, walishamaliza na wapo kambini kuendelea kushuti muvi hiyo.
Kwa upande wake Mtitu alipotafutwa kuhusiana na sakata hilo, alikiri kutokea na kudai walishayamaliza ingawa hapendi kulizungumzia kwa undani suala hilo.
No comments:
Post a Comment