Chunusi ni tatizo sugu linalosababishw a na
mambo kadha wa kadha. Tafiti nyingi za kisayansi zimeshafanywa na zinaendelea
mpaka leo kutafuta mbinu au tiba ya haraka kwa tatizo hili.
Kimila, wengi husema chunusi ni dalili ya kutunikiwa kupendwa na mtu aliyeko mbali na usiyemfahamu (secret admirer), eti basi
ndio maana unatokwa na chunusi (tabasamu basi kidogo). Wapo wanaosema zipo chunusi
za kupevusha yai la hedhi kwa wanawake na wasichana pindi tarehe za mzunguko wake
zinapokaribia.
Chunusi za namna hii humtoka
mtu kamoja tu na kuwa haijifichi kabisa huku
chache huwatoka katika masikio na wengine
ndani ya pua.
Matokeo ya tafiti za kisayansi za kiutaalam
imegundua kwamba chunusi husababishwa
na kuongezeka kwa uzalishwaji wa
'Testosterone hormone' na mafuta ya mwili
'sebum' wakati wa mabadiliko ya kimwili
(Sebum ni aina ya mafuta kama nta yanayozaliwa kwenye vinyweleo chini ya
ngozi yako). Chunusi pia husababishwa na
msongo wa mawazo, matatizo ya kisaikolojia
pamoja na lishe iliyojaa sukari nyingi na
mafuta.
Bidhaa kama Manjano (Turmeric),
giligilani, nyanya, ndimu, Aloe Vera, Zinc na
Vitamin ‘A’ ni vitu vya asili vinavyo weza kutibu chunusi. Kuna baadhi ya bidhaa ambazo hazishauriwi kutumiwa hasa kama
mtu unatatizo la kiafya au mjamzito hivyo unatakiwa kuwasiliana na daktari wako kwa
ushauri kabla ya kutumia hizi vitamin nadawa.
T1PS MUHIMU ZA KUZINGATIA
1. Hakikisha unaacha kama sio unapunguza
vyakula vyenye mafuta sheteshete na sukari
nyingi mpaka utakapomaliza tiba yako. Mfano
chipsi, vitumbua, chapati, keki, biskuti, pipi,
soda, nk uviache au upunguze mpaka
utakapopona chunusi.
2. Umeshasikia mara nyingi kuwa “maji ni
tiba”, jenga tabia ya kunywa maji angalau
glasi 8 kwa kutwa nzima
3. Osha uso wako mara mbili kwa siku.
Usinawe uso wako mara kwa mara kama
samaki. Tumia sabuni iliyoandikwa ‘mild
soap’ (mfano Protex Acne Soap au gentle
facial wash) na maji ya vuguvugu wakati wa
kuosha uso wako.
4. Tumia cream au lotion yenye ‘benzoyl
peroxide’ ndani yake. Ukienda pharmacy
(duka la dawa) unaweza kuulizia kwa
muhudumu.
5. Usijaribu kuzitumbua chunusi mwenyewe
maana unaweza kusukuma ‘infection’
ikaingia zaidi ndani ya ngozi yako ambayo
itasababisha uvimbe mwingine na wekundu
kujitokeza. Kama unataka kuzitumbua
chunusi zilizoiva ni vyema uende ‘Professional
salon’ ukafanyiwe ‘facial treatment’ kitaalam.
6. Kama unahitaji kuondoa chunusi kwa ajili
ya shughuli maalum kama harusi au mkutano
ukiwa kama mtoa mada, nenda kwa daktari
wa ngozi ‘dermatologist’ akusaidie
kukupatia tiba ya chapchap. Maana anaweza
kukuandikia dawa za antibiotics za kumeza
au za kupaka – itategemea na hali ya chunusi
na ngozi yako.
7. Jaribu kujizuia kugusa uso wako na
mikono kila mara. Ukiwa unaongea kwenye
simu jaribu kuzuia simu isiguse uso wako –
kunaweza kukawa na ‘sebum’ juu ya ngozi
yako itakayokuathiri .
8. Hakikisha unanawa mikono yako mara kwa
mara kila unapotoka chooni au kila baada ya
masaa kadhaa. Unaweza pia kutumia
‘antibacterial hand gel’. Mikono yako mara
zote iwe misafi.
9. Unapotaka kugusa uso wako mara zote,
hakikisha umenawa mikono yako na sabuni
hasa kabla ya kupaka lotion, cream au make-
up.
10. Kama una vaa miwani, inatakiwa
zipanguswe mara kwa mara maana zinaweza
zoa 'sebum' kwenye ngozi yako.
11. Ngozi yako intakiwa ipumue. Kama
chunusi ziko mgongoni, kwenye mabega au
kifuani, hakikisha unavaa nguo zisizobana.
Kama inakubidi kuvaa nguo za kubana
hakikisha ni safi na unazifua mara kwa mara.
12. Usiende kulala na make-up usoni. Tumia
make-up isiyokuwa na mafuta au soma label
iliyoadikwa ‘Oil free’.
13. Nywele zako zinazogusa usoni ziwe safi
wakati wote au zisiguse uso wako kabisa
maana na zenyewe pia zina uwezo wa kuzoa
‘sebum’ na kuambukiza sehemu zingine
ambazo chunusi hazijatokea.
14. Epuka na jua kali maana mionzi mingi ya
jua kwenye uso au ngozi yako huleta jasho na
kuzalisha ‘sebum’.
15. Hakikisha foronya ya mto wako
unabadilisha kila baada ya siku moja au mbili.
Inashauriwa kama una chunusi zifuliwe kila
siku - hasa kama usiku unatokwa na jasho
usoni wakati wa kulala. Kuna uwezekano
mkubwa wa ‘sebum’ kubakia kwenye foronya
na kuambukiza sehemu zingine za ngozi yako.
No comments:
Post a Comment