Thursday 23 January 2014

Kesi ya Ubakaji ya Ribery na Benzema Yaanza Kusikilizwa Ufaransa

Wacheza soka wawili mashuhuri duniani wa timu ya taifa ya Ufaransa, wamefikishwa mahakamani mjini Paris Ufaransa kwa kosa la kufanya ngono na kahaba aliyekuwa na umri mdogo.
Msichana huyo mwenye umri wa miaka 21 sasa hivi, alisema kwamba,Franck Ribery, mchezaji wa Bayern Munich , alimtumia kama zawadi wakati wa sherehe za siku yake ya kuzaliwa mwaka 2009.
Inaripotiwa Ribery alimkatia msichana huyo tiketi ya ndege aweze kusafiri kutoka Ujerumani Kuja Ufaransa kumtumbuiza Ribery wakati wa sherehe hizo.
Alisema kuwa pia alilipwa ili afanye ngono na Karim Benzema anayecheza soka yake na klabu ya, Real Madrid.
Kahaba huyo alisema kwamba, aliwaambia wawili, hao kuwa alikuwa mtu mzima wakati huo.
Benzema amekanusha madai ya msichana huyo.
Wachezaji hao wanaweza kufungwa jela miaka mitatu kila mmoja ikiwa watapatikana na hatia.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...