Thursday 23 January 2014

HUYU NDIYE MSANII WA BONGO MOVIE ANAYESEMA HAWAJUI WEMA SEPETU NA JACKLINE WOLPER NDIYO WAKINA NANI...!!

MUIGIZAJI wa kike aliyetamba katika Tamthiliya ya Jumba la Dhahabu, Cecilia Sospeter ‘Mamtei’ ametoa kali ya aina yake baada ya kusema hawajui wasanii kutoka Bongo Movie, Wema Sepetu na Jacqueline Wolper. 
 
Cecilia Sospeter ‘Mamtei’.
Muigizaji huyo aliyejifungua mtoto wake wa pili wiki kadhaa zilizopita, aliyasema hayo juzikati alipokuwa akihojiwa na paparazi wetu nyumbani kwake Kinondoni, jijini Dar na alipogusiwa kuhusu uwezo wa Wolper na Wema, alitiririka:

 
Jack Wolper.
“Wolper ndiyo nani na huyo Wema ndiyo nani? Wala siwajui kabisa na ndiyo kwanza nawasikia kutoka kwako. Bongo Movie imevamiwa kwa sasa na ndiyo maana wengi wanaoonekana ni wafanyabiashara na si waigizaji,” alisema Mamtei.

Wema Sepetu.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...