Tofauti ya ubongo wa mwanamke na wa mwanaume. (Human brain analysis) - By Giningi Siyabonga (Braza Joni)
1. Ubongo wa mwanamke unaweza kufanya mambo mawili kwa wakati mmoja;
mfano kuzungumza kwenye simu na kufuatilia kipindi kwenye TV. Mwanaume
hawezi. 2. Lugha: wanawake wanaweza kujifunza lugha nyingi
kwa urahisi. Chukua mtoto wa kike na wa kiume wenye umri wa miaka
mitatu. Mara nyingi wa kike atakuwa anajua maneno mengi kuliko wa kiume.
3. Kusema uongo: mwanaume akimdanganya mwanaume uso kwa uso ni rahisi
kushtukiwa. Wanawake hugundua ukweli kupitia uso wako kwa 70%, kupitia
body language yako 20% na 10% kupitia maneno yako. Ubongo wa mwanaume
hauna uwezo wao ndiyo maana ni rahisi mwanamke kumdanganya mwanaume uso
kwa uso. Guys, next time ukiwa unamdanganya msichana ni better mkiwa
hamko uso kwa uso. 4. Uwezo wa kutatua matatizo: mwanaume
akiwa na matatizo, ubongo wake huyachukua na kuyatenga katika makundi
mbalimbali na kisha huanza kutafuta suluhisho moja baada ya jingine.
Mwanamke akiwa na matatizo ubongo wake hauwezi kuyatenga na badala yake
hutaka mtu amsikilize. Baada ya kumwambia mtu matatizo yake yote akili
yake hupata kiwango fulani cha utulivu na huwa mara nyingi hajali kama
yatatuliwa au la. 5. Mahitaji: Wanaume wanahitaji heshima
kwenye jamii, mafanikio, sifa, nk.; wanawake wanapenda mahusiano,
familia, marafiki, etc. 6. Kuongea: mwanamke mara nyingi hutumia lugha ya kificho. Mwanaume hutumia lugha ya moja kwa moja. CHANZO NI MASANJA MKANDAMIZAJI: |
No comments:
Post a Comment