Tuesday 11 June 2013

MAZISHI YA MWIGIZAJI JAJI KHAMIS ( KASHY) YAFANYIKA LEO


Mazishi ya mwigizaji mwigizaji Jaji Khamisi (Kashi) aliyefariki jana mchana kwenye hospitali ya muhimbili jijini Dar es Salaam yamefanyika leo mchana majira ya saa nane kwenye makaburi ya kinondoni jijini Dar es Salaam.
Marehemu alikubwa na umauti baada ya kuugua ghafla malaria na kifua vilivyosababisha kufikwa na mauti hayo.
 Mazishi hayo ambayo yalihudhuriwa na waigizaji wengi wa tasnia ya bongo movies yalitawaliwa na huzuni ikizingatiwa kuwa mwanadada Kashi alikuwa ni mtu asiye na tatizo lolote na mtu na ni mtu aliyekuwa mpole na mwenye upendo na watu wote.
Kabla ya kufariki marehemu  alikuwa akiishi maeneo ya Kinondoni Mkwajuni  na mume wake na ndipo msiba wake ulipokuwa kwa siku hizi mbili.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi amina.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...