Tuesday 11 June 2013

KUNDI LA MAKHIRIKHIRI LA NCHINI BOTSWANA WASHTUSHWA NA KIFO CHA MANGWAIR! HII NDIO KAULI WAIYOITOA

 Kiongozi wa kundi la Makhirikhiri toka nchini
 Botswana  Shumba Ratshega



Marehemu Arbeth Mangwair

Kiongozi wa kundi la Makhirikhiri toka nchini Botswana Moses Marapela a.k.a Shumba Ratshega amesikitishwa na msiba wa mwanamuziki Alberth Mangwair na kusema kifo hicho ni pigo kubwa sana ndani ya kundi lake kwa vile tayari walikuwa na michakato ya kuja kufanya kazi pamoja.
Akiongea Xdeejayz rafiki wa karibu wa mwanamuziki huyo Livingstone Mkoi alisema " Ni kweli shumba amenipigia simu toka nchini Denmark ambako kundi hilo liko nchini humo kwa ziara ya kimuziki na kutoa pole kwa familia ya marehemu na kwa watanzania kwa ujumla" Alisema Mkoi
Aidha katika hatua nyingine Shumba aliongeza kusema kuwa alimfahamu marehemu pindi alipokuja nchini mwaka juzi na walizungumza mambo mengi ikiwa na pamoja na kuja kufanya kazi pamoja siku za usoni. 
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...