Kutokana na hilo FA aliamua kufunguka; “Tunaishi na watu hivyo lazima mtagongana, hata mapacha wanakosana na kusameheana, lakini wakati mwingine shida inawafanya mnapatana,” alisema Mwana FA.
Mwanamuziki
Hamis Mwinjuma, maarufu Mwana FA, amepata wakati mgumu kwa
kulazimishwa na mashabiki kutaja jina la Lady Jay Dee, baada ya
kuliruka jina hilo alipokuwa akiimba wimbo wa Mabinti ambao ndani yake
kuna jina la Jay Dee.
kuna jina la Jay Dee.
Tofauti
na ilivyozooeleka katika wimbo wa Mabinti, kwa mara ya kwanza Mwana FA
aliruka jina la mwanamuziki Lady Jay Dee ‘Anaconda’, hali iliyowafanya
mashabiki wamtake arudie tena na kutenda haki.
Mwana
FA alisita kwa muda na baadaye aliamua kurudia wimbo huo na alipofika
katika kipengele cha kumtaja Jide aliimba kwa kumtaja, hali iliyoufanya
ukumbi huo ulipuke kwa shangwe na mashabiki kumtaka arudie tena na
tena.
Kutokana
na hilo FA aliamua kufunguka; “Tunaishi na watu hivyo lazima
mtagongana, hata mapacha wanakosana na kusameheana, lakini wakati
mwingine shida inawafanya mnapatana,” alisema Mwana FA.
Awali
shoo ilitangazwa kuwa ingekuwa ya watu 400 tu. Lakini mpaka inafika
saa nne kasoro usiku, muda uliotangazwa kuanzwa kwa shoo hiyo watu
waliokuwa wamefika walikuwa kama 250 tu.
No comments:
Post a Comment