Monday 10 June 2013

AMINI AKANA KUJIFUNGIA NDANI ALIPOMWAGANA NA LINAH

KUPITIA Kiti cha Moto Msimu Mpya utamsikia staa wa Bongo Fleva kutoka Nyumba ya Kukuza Vipaji Bongo ‘THT’, Amini Mwinyimkuu akifunguka laivu juu ya maswali mliyomuuliza wiki iliyopita. TAMBAA NAYO...
Amin akiwa na Linah.
NJE YA FANI
Kaka mbali na usanii wa muziki unafanya kazi gani nyingine? Joseph, Dar, 0755708366
AMINI: Nina biashara zangu ambazo siwezi kuziweka hadharani!

UHUSIANO NA LINAH
Amini uhusiano wako na Linah (Estalina Sanga) uko kama kulipa fadhila za kumsaidia kimuziki au? Msomaji, 0718185998
AMINI: Linah hanilipi fadhila kwa sababu nimeumbwa kumsaidia kila mtu na nimewasaidia wengi. Kuhusu Linah, hivi karibuni nitatoa tamko rasmi.

USHAURI
Pongezi nyingi sana zikufikie kwako hapo ulipo best, kaza buti na usikate tamaa hata kidogo maana tumeshakuzoea sasa, ukiwa kimya unatuacha njia panda. Prosper Mallya, Kilimanjaro, 0658565860
AMINI: Usijali kazi zinakuja nyingi sana.

LINAH TENA
Amini au Super Voice kama ninavyopenda kukuita, wewe ni bonge la mwimbaji, nilipata tetesi kuwa ulivyomwagana na mpenzi wako Linah ulikuwa unajifungia ndani kutwa nzima bila kutoka nje. Raphael, Morogoro, 0713850820
AMINI: Siyo kweli.

TULIZANA
Napenda kukushauri Amini, tulizana katika suala la mapenzi kwani hayahitaji kukurupuka. Amiri Salumu, Dar, 0653252416
AMINI: Sawa nishatulizana.

MAPENZI YAPO TU!
Dogo tulizana maisha ni kama kamari, mapenzi yapo na yataendelea kuwepo, mwanamke anayekuzingua achana naye usimbembeleze. Amos Msigwa, Iringa, 0752544722
AMINI: Nakupa tano.

YEYE NA MWASITI
Amini wewe ni mkali kaka, hongera sana, kuhusu Linah vipi nasikia unataka kumuoa unamuacha Mwasiti (Almasi) tena? Lovenes, 0716305399
AMINI: Siyo kweli, sijawahi kuzungumzia kuhusu kuoa. Mwasiti ni dada yangu kama walivyo dada wengine.

KAZI NA LINEX
Nakupenda sana, kiukweli una sauti ya kuimba, napenda ufanye kazi na Linex (Sunday Mangu). Kalvin, 0758277747
AMINI: Sawa nitalifanyia kazi na tulishaandika wimbo bado kuutoa tu.

LINAH ALICHEZEA BAHATI?
Mimi nakupongeza Amini kwani ni mwanaume usiye na kashfa na ninahisi una mapenzi ya dhati, naona Linah alichezea bahati. Deborah, Dar, 0713306515
AMINI: Nashukuru sana.

YEYE NA MTOTO WA WAZIRI
Inasemekana ulivyoachana na Linah ulitoka na mtoto wa waziri, je, ni kweli? Alice, Dar, 0659260109
AMINI: Sijawahi na simjui.

VIPI ANASAIDIA CHIPUKIZI?
Amini una mpango wowote wa kuwasaidia wasanii chipukizi labda baadaye au hata sasa hivi, kama ipo nafasi hiyo ya kuwasaidia naomba utuwekee namba yako wazi. Msomaji, 0656127124
AMINI: Nawasaidia kimawazo, kuhusu kuweka namba, nitaitoa siku nyingine.

ALIJIPIGA DONGO?
Nilisikia uhusiano wako na Linah ulishafika mwisho wa reli, je, ni kweli wimbo wa Bora Nikimbie wa Linah ulikuwa ni dongo kwako? Iddi Mayunga, Dar, 0766185177
AMINI: Wimbo huo mimi ndiyo mtunzi hivyo huwa nacheza na nyakati na kuangalia mashabiki wanataka nini kwa wakati huo kwa hiyo siwezi kujipa dongo mwenyewe.

BIFU NA BARNABA KISA LINAH!
Mimi nakukubali kama ulivyo, eti nasikia una bifu na Barnaba (Elias) kisa Linah. Brightnes, 0757325435
AMINI: Watoto wa THT siku zote hatuna mabifu.

ELIMU VIPI?
Naomba kukuuliza kuhusu kiwango chako cha elimu, umefikia wapi? Msomaji, 0758340325
AMINI: Suala hilo ni binafsi siwezi kulizungumzia.

HISTORIA KWA KIFUPI
Kaka Amini ningependa kujua historia yako kwa ufupi. Hp, Dar, 0654766145
AMINI: Mimi ni mtoto wa mwisho kati ya saba tuliozaliwa katika familia yetu, nina kipaji cha kuimba na kucheza mpira, nina miaka 13 kwenye muziki, nimezaliwa Hospitali ya Mwananyamala, Dar mwaka 1986.

USHAURI
Amini mimi naamini wewe ni msanii mwenye kipaji cha kipekee, Musoma kuna wasanii wengi wenye vipaji wameshindwa kutoka kutokana na studio za huku kutokujitosheleza vifaa pia kutokuwa na mkwanja wa kuja kurekodi huko Dar, je, unatusaidiaje? Chozy, Musoma, 0753749950
AMINI: Mtafutaji hakosi kama mnajiamini mko vizuri endeleeni kufanya mazoezi msichoke kutafuta, nendeni kwenye matamasha, fanyeni shoo msijali fedha kwanza.
ANATOKEA MKOA GANI?
Amini wewe ni mzaliwa wa mkoa gani? Julius, Songea, 0713199777
AMINI: Asante, mimi ni mzaliwa wa Dar, baba yangu ni mtu wa Lindi na mama ni mtu wa Msumbiji.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...