Tuesday, 7 May 2013

Mwenyekiti wa chama Cha NCCR-Mageuzi katika Wilaya ya Ngara mkoani Kagera, Kenned Staford Festo Ajiuzulu

Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi na mbunge wa kuteuliwa James Mbatia
--
Mwenyekiti wa chama Cha NCCR-Mageuzi katika Wilaya ya Ngara mkoani Kagera, Kenned Staford Festo amejitoa katika uongozi wa chama hicho kwa madai kuwa chama hicho kimekosa mwelekeo katika kuwahamasisha wanachama na wananchi kwa ujumla kuondoa changamoto zao katika kujipatia maendeleo wilayani humo.
Mwenyekiti huyo amechukua uamuzi huo jana baada ya kamati tendaji ya chama hicho mkoani Kagera kumsimamisha kwa muda wa miezi miwili iliyopita tangu Februari 20 mwaka huu ikidaiwa alishiriki maadhimisho ya miaka 36 ya CCM wilayani Ngara.
Akitangaza kujiuzulu Mei 2, Staford alisema amechoka kutumikia chama kisicho na ruzuku ya kuchangia maendeleo na ametumia gharama nyingi kuwahudumia wanachama huku akikosa nguvu kutoka kwa viongozi ngazi ya taifa akiwamo Katibu wa Chama hicho Taifa, Samweli Ruhuza. (Shaaban Ndyamukama) 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...