Monday, 6 May 2013

LIGIKUU SOKA NCHINI ENGLAND INAZIDI KUELEKEA UKINGONI KWA TIMU KUCHEZA MICHEZO YA MWISHONI

Jumapili ya jana kulichezwa michezo miwili pekee,
Manchester United walikuwa nyumbani kuwakaribisha Chelsea The blues kwenye uwanja wa Old Traford, wakati Liverpool walikuwa kwenye uwanja wa nyumbani kupambana na watani zao wa jadi, Everton.
Katika mchezo ambao BBC Ulimwengu wa soka ilikuwa ukiutanga moja kwa moja, United walijikuta wakilala kwa bao moja ka bila katika mchezo ambao ulikuwa hauna mashamu shamu kama wengi walivyotarajia.
Bao hilo la Chelsea lilifungwa na Kiungo Mhispania Juan Matta dakika ya 87 baada ya kuachia shuti la wastani lililomgonga beki wa United Phil Jones na kuwafanya mashabiki wa United kukaa kimya uwanjani.
Katika mchezo huo United walimaliza wakiwa pungufu baada ya Rafael Da Silva kupewa kadi nyekundu dakika chache kabla ya mchezo kumalizkka baada ya kumkwatua beki wa Chelsea David Luiz ambaye ni mbrazil mwenzake.
Matokeo haya yanaifanya Chelsea kupanda hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu wakiwa na pointi 68 huku Arsenal wakishuka hadi nafasi ya nne na pointi 67 na Tottenham wakishika nafasi ya tano na pointi 65. Chelsea itapambana na Tottenham hapo jumatano usiku katika mechi itakayokuwa na upinzani mkubwa kwa timu zote mbili kusaka uwezekano wa kumaliza kwenye nne bora ya ligi kuu soka nchini England.
Katika mchezo mwingine wa mapema, Everton walikuwa wageni wa Liverpool katika mchezo wa watani wa jadi wa mji wa Merseyside.
Mapema Sylivan Distin alifunga bao kwa kichwa lakini mwamuzi Michael Oliver alilikataa kwa kuwa Victor Anichebe wa Evrton alimchezea vibaya golikipa wa Liverpool Pepe Reina.
Everton hawajawahi kushinda kwenye uwanja wa Anfield tangu mwaka 1999 katika mechi za watani wa jadi na Liverpool za ligi kuu soka nchini England.
Mechi ya leo ya sare ya Liverpool na Everton inatimiza idadi ya michezo 35 ya kutoka sare katika ligi kuu soka nchini England.
Ligi hiyo itaendelea tena hapo kesho jumatatu kwa mchezo mmoja kati ya Sunderland watakao wavaa Stoke City.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...