Mwakilishi
wa Kampuni ya Kimataifa ya Kibiashara ya Shanfar & Patners ya Mjini
Salala Nchini Oman Bw. Ali Omar Al-Sheikh akizungumza na Makamu wa Pili
wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisini kwake Vuga Mjini
Zanzibar.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Ujumbe
wa Viongozi watano wa Kampuni ya Kimataifa ya Kibiashara ya Shanfar
& Patners ya Mjini Salala Nchini Oman uliofika ofisini kwake.
Balozi
Seif akiiomba Kampuni ya Kimataifa ya Kibiashara ya Shanfar &
Patners ya Mjini Salala Nchini Oman kupitia Mwakilishi wake Bw. Ali Omar
Al-Sheikh kutumia fursa zilizopo za rasilmali Zanzibar kuwekeza vitega
uchumi vyao Nchini.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Mwakilishi wa
Kampuni ya Kimataifa ya Kibiashara ya Shanfar & Patners ya Mjini
Salala Nchini Oman Bw. Ali Omar Al-Sheikh wakibadilisha mawazo katika
masuala ya uwekezaji Zanzibar.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika picha ya
pamoja na ujumbe wa Viongozi watano wa Kampuni ya Kimataifa ya
Kibiashara ya Shanfar & Patners ya Mjini Salala Nchini Oman baada ya
mazungumzo yao yaliyohusu suala la uwekezaji hapa Nchini. (Picha na
Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ).
Kampuni
ya Kimataifa inayojishughulisha na masuala ya Kibiashara ya Shanfar
& Partners Co. L.L.C yenye Makao makuu yake Mjini Salala Nchini
Omar imeonyesha nia ya kutaka kuwekeza vitega uchumi vyake Zanzibar.
Nia
hiyo imekuja kufuatia Visiwa vya Zanzibar kubarikiwa kuwa na rasilmali
kadhaa ambazo bado hazijatumika katika kusaidia kuendeleza uchumi wa
Taifa sambamba na kuongeza vipato kwa wananchi.
Mwakilishi
wa Kampuni hiyo Bw. Ali Omar Al–Sheikh akiuongoza ujumbe wa Viongozi
watano wa Kampuni hiyo alieleza hayo wakati akizungumza na Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisini kwake Vuga Mjini
Zanzibar.
Bw.
Ali Omar amesema ujumbe wake umeridhika na rasilmali kadhaa zilizomo
ndani ya Visiwa vya Zanzibar baada ya kupata fursa ya kutembelea maeneo
mbali mbali Mijini na Vijijini.
Amefahamisha
kwamba Taasisi yao itaangalia maeneo inayoweza kuwekeza baada ya
kufanya uchambuzi wa kina wakilenga zaidi katika Sekta ya Utalii ambayo
Zanzibar tayari imeshafikia hatua kubwa katika kuimarisha miundo mbinu
ya sekta hiyo.
Naye
Ofisa Mkuu wa Kampuni hiyo ya Shantar & Partners Bw. S. Srihar
amemueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba katika jitihada za
kusaidia maendeleo ya Zanzibar Kampuni yao ina uwezo wa kuyashawishi
mashirika na Makampuni ya Kimataifa ya watembezaji Watalii kulitumia
soko la Zanzibar la Utalii katika kutembeza wateja na wageni wao.
Bw.
Srihar amesema kufanikiwa kwa mpango huo kunaweza kutoa nafasi ya ajira
kwa wazalendo waliowengi Nchini hasa lile kundi kubwa la vijana
wanaomaliza masomo yao.
Akitoa
shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
aliueleza Ujumbe huo wa Kampuni ya Shanfar & Partners ya Salala
Nchini Oman kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar bado inaendelea na
juhudi za kuimarisha miundo mbinu katika sekta mbali mbali za Kiuchumi
hapa Nchini.
Balozi
Seif alifahamisha kwamba uimarishaji wa kiwanja cha ndege cha
Kimataifa cha Zanzibar ni miongoni mwa hatua hizo kwa lengo la kujenga
mazingira mazuri ya uwekezaji.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliushauri Ujumbe huo wa Kampuni ya
Kibiashara ya Shanfar & Partners kuitumia fursa hiyo ili isaidie
uchumi wa Zanzibar sambamba na kuimarisha uhusiano wa Kihistoria uliopo
kati ya Zanzibar na Oman.
Kampuni
ya Kimataifa ya Kibiashara ya Shanfar & Patners Co. L.L.C ya
Salala Nchini Oman imekuwa na ubia wa kibiashara na zaidi ya Makampuni
saba ya Kimataifa katika Nyanja za Viwanda, Usafiri wa Anga, Utalii,
huduma za Umeme, ujenzi na Uchapishaji.
Chanzo brownbreez.blogspot.com
No comments:
Post a Comment