Jacqueline Wolper Massawe.
STAA wa filamu za Kibongo,
Jacqueline Wolper Massawe anadaiwa kutupiwa nje na baadaye kuzuiliwa
vyombo vyake kwenye ile nyumba ya kifahari ya kupanga aliyokuwa akiishi
Mbezi Beach, Dar es salaam.
Madai hayo yalitua kwenye dawati la
GPL hivi karibuni ambapo ilielezwa kuwa ishu hiyo ilijiri maeneo hayo
baada ya bishosti huyo kudaiwa kuwa alishindwa kulipa kodi ya pango ya
mwezi mmoja ambayo ni Dola 1,500 (zaidi ya Sh. milioni 2.4 za madafu).
Kwa mujibu wa ‘sosi’ wetu
aliyekuwepo eneo la tukio, Wolper aliwatuma ndugu zake kwenda kuchukua
vyombo hivyo lakini walipofika mama mwenye nyumba (jina tunalo),
aliwazuia na kumpigia simu staa huyo akimwambia kuwa anatakiwa kulipa
fedha kabla ya kuchukua vitu vyake.
“Wolper alipopigiwa simu alikuja juu
na kumwambia mama mwenye nyumba kuwa kama anamfuatilia eti atamfunga
kama mume wa mama huyo alivyofungwa na kumwambia kuwa atampelekea polisi
wakamkamate,” alidai mtu huyo.
Sosi huyo aliendelea kudai kuwa
baada ya kuona soo limekuwa la kutishana, mama huyo alikwenda kumfuata
mjumbe wa nyumba kumi aliyefahamika kwa jina moja la Musa na kumueleza
kisha kumuomba asimamie zoezi hilo.
Baada ya kujazwa data hizo, GPL
ilifanya jitihada za kumsaka Wolper na alipopatikana alisema kuwa
hajawahi kudaiwa na huyo mama na anayesema hivyo huenda alimuona wakati
anahamisha vitu vyake kwani kwa sasa amehama kwenye nyumba hiyo.
Mwandishi wetu hakuishia hapo,
alimtafuta shemeji wa mama mwenye nyumba aliyetajwa kwa jina moja la
Jamal ambaye alikiri kutokea kwa ishu hiyo na kwamba suala hilo
lilimalizika ambapo vyombo vya Wolper vilitolewa kwa ajili ya kufanya
usafi kwani kuna mtu mwingine alikuwa akihamia.
Mjumbe wa Nyumba Kumi, Musa
alipotafutwa kwenye simu yake ya kiganjani ili kuzungumzia sakata hilo
alikiri kufikishiwa malalamiko ya Wolper.
Alisema kuwa msanii huyo alikuwa
hajamaliza kulipa fedha, akawatuma ndugu zake wakachukue vitu vyake
lakini kabla hawajavichukua mama mwenye nyumba aliwazuia mpaka alipwe
chake na alipotimiza hilo ndipo akaachiwa vitu vyake
No comments:
Post a Comment