Afisa
Utamaduni Jiji la Tanga, Peter Semfuko (katikati) ,Matron Hilda Mwinyi
(Kulia), na Mratibu wa kamati ya maandalizi Kessy Salum Mbasha (Kushoto)
wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa fainali za taifa za Miss
Utalii Tanzania 2013, alipo kwenda kukagua kambi na kuzungumza na
warembo hao Jana katika hoteli ya Mwambani Tanga Beach.
Afisa
Utamaduni Jiji la Tanga, Peter Semfuko (katikati) ,Matron Hilda Mwinyi
(Kulia), na Mratibu wa kamati ya maandalizi Kessy Salum Mbasha (Kushoto)
wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa fainali za taifa za Miss
Utalii Tanzania 2013, alipo kwenda kukagua kambi na kuzungumza na
warembo hao Jana katika hoteli ya Mwambani Tanga Beach.
Wakati
Maandalizi ya fainali za taifa za Miss Utalii Tanzania 2013 yanaendelea
kwa kasi katika hoteli ya kitalii ya Mwambani iliyopo katika ufukwe wa
Tanga, huku kila Mrembo akijifua vikali, Afisa Utamaduni wa Mkoa wa
Tanga Ndugu Peter Semfukwe ametembelea kambini hapo, kujionea yeye
mwenyewe warembo wa Miss Utalii Tanzania 2013 ambao wanajiandaa na
Fainali hizo za Taifa zitakazo fanyika wiki Ijayo,kasha alizungumza nao
na kuwakaribisha mkoani Tanga.
Afisa
Utamaduni alisema kuwa amefurahi kukutana na warembo wote wakiwa
katika Afya Njema, Mvuto na kila mmoja kuonekana ndiye atakaye twaa taji
hilo la Miss Utalii Tanzania 2013, pia ameipongeza kamati ya maandalizi
kwa juhudi na jitihada kubwa za kuandaa mashindano hayo ambayo dhima
yake ni kuutangaza utalii wa ndani pamoja na utamaduni wa Mtanzania.
Aliongeza kuwa anaahidi ushirikiano mkubwa wa hali na mali wakati wa
maandalizi mpaka mwisho wa mashindano hayo.
Akizungumza
na Warembo wa Miss Utalii Tanzania 2013 pamoja na Kamati ya Maandalizi
ya Miss Utalii Tanzania , Afisa Utamaduni aliwaasa warembo hao wawe na
heshima, adabu, na pia wawe ni mfano bora wa kuigwa katika jamii ikiwa
ni warembo hao kuwa mstari wa mbele katika kushiriki, kutangaza Utalii
na Utamaduni wa Mtanzania.
Mpaka
sasa Kambi ya Miss Utalii Tanzania 2013 ipo jijini Tanga Mwambani Hotel
na inaendelea Vizuri, Warembo zaidi ya 30 kutoka mikoa yote nchini
,wanajiandaa vizuri kwa ajili ya Fainali Hizo zitakazo fanyika wiki
ijayo Tanga, Kanda Maalum ya Zanzibar na Vyuo vikuu Tanzania.
Akizungumzia,
juu ya maendeleo ya kambi, Fredy Njeje, alisema kuwa baada ya
kukwamishwa na wadhamini walio toa ahadi hewa, wamelazimika kuhamishia
shindano hilo mkoani Tanga,baada ya kuvutiwa na mwamko wa wafanya
biashara na makampuni ya Jiji la Tanga wa kuwa na uwezo wa kudhamini
matukio makubwa ya kitaifa na kimataifa.
Tunakabiliwa
na changamoto ya warembo wengi kuwa wapya katika kambi yetu,baada ya
wale waliokuwako kambini kabla ya kambi kuahirishwa kushindwa kurudi
kambini kwa sababu mbalimbali,zikiwemo za kimasomo na wengine kukata
tama baada ya kuahirisha. Hata hivyo tayali nafsi zao zimechukuliwa na
washindi wa pili wa mikoa yote ambayo warembo wake wameshindwa kurudi
kambini, na tayali warembo 30 wameripoti kambini na tunategemea wengine
10 kuripoti kambini wakati wowote ili kufikisha idadi ya warembo 40 wata
kao panda jukwaani. Tumejiandaa na tunapata ushirikiano mkubwa kwa
serikali ya mkoa nay a Jiji la Tanga, hivyo kutuhakikishia kuwa tarehe
itakayo pangwa sasa haitabadilika tena wala kuahirishwa. Tarehe kamili
ya shindano itatangazwa kesho na mwenyekiti wa kamati ya maandalizi
ambaye pia ni Afisa Utamaduni wa Jiji la Tanga.
Washindi
wa 1-5 wa Fainali za Taifa ,watawakilisha Tanzania katika mashindano
mbalimbali ya Dunia na nchi yatakako fanyika katika mabano
International Miss Tourism World (Marekani), Miss Tourism United Nation
(Mexico), Miss Heritage World (Tunasubiri Taarifa), Miss Tourism
University World(Tanzania), Miss Globe International (Uturuki), Miss
Tourism World ( Equatorial Guinea ), Miss Freedom Of The World ( Kosovo)
, na Miss Tourism United Nation (Nigeria) n.k
Wakati huohuo, katika kuhakikisha kuwa maandalizi ya Fainali za taifa,
za mashindano hayo ambapo mkoa wa Tanga unakuwa wenyeji kwa mara ya
kwanza yanafanyika kwa ubora na hayakwami, kamati ya maandalizi ya
kimkoa umeundwa ambayo mwenyekiti wake ni Peter Semfuko Afisa Utamaduni
wa Jiji la Tanga. Miss Utalii Tanzania ,hadi sasa tunashikilia Jumla ya
mataji 5 ya Dunia na kimataifa, yakiwemo ya Miss Tourism World
2005-Africa,Miss Tourism World 2006-SADC,Miss Tourism World 2007-Africa,
Miss Tourism
Model Of The World 2008-Personality, Miss Africa 2006 – 1ST Runner Up n.k
No comments:
Post a Comment