Mwanaume mmoja Mtanzania amekamwata katika uwanja wa kimataifa wa
Jomo Kenyatta Nairobi Kenya akiwa amebeba dawa za kulevya akiwa njiani
kuelekea Antananarivo ambapo mzigo huo ulitokea Tanga kisha ukapita
Mombasa na baadae kwa ndege mpaka Nairobi.
Mzigo wenyewe ni wa cocaine na Heroin ambazo zote zina thamani ya zaidi
ya shilingi milioni 24 za Kitanzania na dawa hizo alikua ameziingiza
katika njia ya haja kubwa.
Mkuu wa kitengo cha CID katika uwanja huo Joseph Ngisa amesema mshukiwa
alikamatwa JKIA na akawekwa kwenye chumba cha uchunguzi na baadae akatoa
tembe za cocain na tembe za Heroin na tayari ameshapelekwa Mahakamani.
Mwezi March mwaka huu watanzania wanne walikamatwa katika uwanja huohuo
walipopatikana na heroin yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 75
za Kitanzania na wote walifikishwa mahakamani na kukiri kosa.
Wanawake watatu na mwanaume mmoja kila mmoja akishtakiwa kando kwa kosa
la kusafirisha dawa za kulevya na walikua wameingia Kenya kupitia
Namanga na walikamtwa wakiwa njiani kuelekea Hong Kong.
Kuanzia March 2014 mpaka leo hii May ni jumla ya Watanzania watano
wamekamatwa kwenye kiwanja cha ndege Nairobi wakiwa kwenye pilika za
kusafirisha dawa za kulevya kwenda kwenye mataifa mengine.
No comments:
Post a Comment