Pati hiyo ilifanyikia ndani ya Hoteli ya Protea iliyopo Masaki jijini Dar na kuhudhuriwa na watu mbalimbali.
MWANADADA ambaye ni mchumba rasmi wa Nasib Abdul ‘Diamond Platnumz’, Peniel Mungilwa ‘Penny’ amemfanyia bonge la pati mama wa Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ ikiwa ni katika kusherehekea siku ya mzazi huyo ya kuzaliwa.
Wakizungumzia pati hiyo, baadhi ya
watu wa karibu wa Penny walisema amefanya kitu kizuri ambacho kinaweza
kumfanya apendwe zaidi ukweni.
“Ameboresha uhusiano wake, unajua kwa
alichokifanya hata akitofautiana na Diamond, mkwe anaweza kumsaidia
kumuombea msamaha,” alisema mmoja wa wasanii wa filamu Bongo

No comments:
Post a Comment