Majina yangu halisi Issaya Lupogo, jina la kisanii Lupogezzle.
Kazi yangu ni mwalimu wa chuo kikuu cha Mzumbe-Tanzania, ila kwa sasa niko masomoni ambapo nafanya digrii ya udhamiri ya Lugha (M.A.Linguistics) katika chuo kikuu cha Dar essalaam.
Muda
wangu wa ziada nafanya sanaa,muziki wa bongo flavour. Nyimbo zangu
ambazo ziko hewani kwa sasa ni "Ufisadi" na "Issaya & Aziza".
Mtazamo wangu wa Muziki hususani muziki wa kizazi kipya:
kufanya muziki huo sio uhuni, uhuni ni tabia ya mtu ambayo hufanywa sio na wasaniii tu bali hata watu ambao tunawaheshimu na kuwaamini katika jamii yetu. Mfano ni mara ngapi tunasikia waheshimiwa wakubwa wamenaswa na vimada? ni mara ngapi tunashuhudia walimu wakiwapa mimba wanafunzi mashuleni.
kufanya muziki huo sio uhuni, uhuni ni tabia ya mtu ambayo hufanywa sio na wasaniii tu bali hata watu ambao tunawaheshimu na kuwaamini katika jamii yetu. Mfano ni mara ngapi tunasikia waheshimiwa wakubwa wamenaswa na vimada? ni mara ngapi tunashuhudia walimu wakiwapa mimba wanafunzi mashuleni.
Malengo yangu katika
muziki wa kizazi kipya (bongo flavour): Kuunganisha wasanii wote wa
Tanzania na kupanga ili tuweze kuwa na chanma chetu cha wasanii
kitakachotambulika ambacho kitatetea haki zetu (Wasanii). Nimejaribu
kuunda kundi ktk Facebook liitwalo "UWABO" Umoja wa Wasanii Bongo,
lakini bado halijapata wadau wengi, kama tujuavyo wabongo kila mtu
anataka kufanya mambo peke yake.
Ushauri wangu kwa wasanii wenzangu:
Wajiamini wsifanye kazi kwa kuogopa. Pia tusijikite kuimba Mapenzi tu,
tuimbe masuala yote yanayolihusu Taifa Letu. Nawapongeza sana wasanii
kama Mrisho Mpoto, Roma na Afande Selle ambao wamekua wakigusa na
sehemu zingine tofauti na mapenzi.
Mwisho: DAWA YA
KUTOKOMEZA UNYONYWAJI NA UONEVU WA WASANII NI KUUNGANA KWA KWA WASANII
WENYEWE NA KUFANYA KAZI KWA PAMOJA HUKU WAKISHIRIKIANA, WAKIJIHESHIMU,
KUSHAURIANA, KUSAIDIANA NA KUPENDANA.
HIZI NDIO BAADHI YA NYIMBO AMBAZO LUPOJIZO AMEFYATUA MPAKA SASA....UNAWEZA KUDOWNLOAD NA KUZISIKILIZA HAPA PIA
No comments:
Post a Comment