
Katika kuzindua msimu mpya wa radio ya Clouds, ambao umefanyika ndani ya
mji mkuu Dodoma, kwa siku tatu mfululizo, Clouds waliandaa semina kwa
ajili ya kuwasaidia vijana, katika uelewa wa fursa zinazotuzunguka na
kujituma kuhakikisha tunatumia fursa hizo kwa maendeleo yetu na taifa
kwa ujumla.
Semina hiyo alifanyika katika ukumbi wa African dream hotel na
kujumuisha vijana wa rika mbali mbali kutoka hapo pamoja na wasanii
waliokuwepo kwa ajili ya shughuli hoyo
wasemaji wakuu siku hiyo walikuwa ni Mh Zitto Kabwe, mwanamuziki Mrisho
Mpoto pamoja na bilionea mwenye umri mdogo 29 {kutokana na forbes},
Patrick Ngowi kutoka Arusha
Patrick Ngowi, mkurugenzi wa kampuni ya Helvetic Solar Contracators
Zenno Ngowi kutoka kampuni ya Tanzania Home Expo
mwanamuziki Mrisho Mpoto
Baada ya semina hiyo kufanyika, watu walielekea uwanja wa Jamhuri kwa
ajili ya sherehe za uzinduzi huo ambapo wasanii mbali mbali walishiriki
katika kutoa burudani kwa maelfu ya raia wa Dodoma waliofika uwanjani
pale

















No comments:
Post a Comment