Taarifa kutoka itv.co.tz imesema Mwanafunzi wa darasa la tatu katika shule ya msingi Kizega wilayani Iramba Mariamu Alphonce mwenye umri wa miaka kumi ameuwawa kikatili kwa kukatwa shingo na kucharangwa kwa panga sehemu mbalimbali za mwili wake na kaka yake aitwae Elibariki Alphonce.
Akieleza
kwa uchungu, Baba wa mtoto huyo Alphonce Msengi amesema alipofika
nyumbani kwenye saa kumi na moja jioni alikuta damu nyingi na alipo
angalia vizuri alimuona mtoto wake Mariamu Alphonce akiwa amekatwakatwa
kwa mapanga na tayari alikuwa ameshafariki.
Baada
ya kuona hivyo alipiga yowe na walikuja majirani na watoto na
wakamwambia tumemuona mtoto wako Elibariki akiwa na mapanga mawili
akikimbia huku akiwa hana nguo ambapo mwenyekiti wa kitongoji Vailet
Mbigu na mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kizega Elisante Gyuzi, wamesema
pamoja na shule kuandaa taratibu zote za mazishi, kijana aliyefanya
huo unyama huwa anavuta bangi na mara nyingi alikuwa akisikika
kumtishia kumuuwa baba yake kwa kumkatakata kwa panga.
Kaimu
mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Iramba daktari Timoth Sumbe
amesema wamempokea Mariamu Alphonce akiwa ameshafariki huku mwili wake
ukiwa na majeraha ya kukatwakatwa sehemu za shingoni na kichwani na
kamanda wa polisi Singida Godfrey Kamwela amethibitisha kutokea kwa hayo
mauaji na kusema jeshi lake linaendelea kumtafuta mtuhumiwa Elibariki
Alphonce.
VIDEO HII HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment