RIPOTI ya Wiki imegundua kuwa akina mama wajawazito wanaotumia draya kukaushia nywele zao wakiwa saluni,wapo katika hatari zaidi kiafya kuliko wale wanaotumia taulo au wanaokausha nywele zao juani.
Matumizi
ya draya kwa ajili ya kukaushia nywele kwa wanawake, yamekuwa kawaida
sana kiasi ambacho wanawake wengi wamejikuta wakitumia bila kujua
madhara yake.
Ukiachilia mbali madhara madogomadogo kama vile kukausha unyevunyevu na mafuta asilia kwenye nywele na kuziacha zikiwa kavu na rahisi kukatika, pia wanawake kadhaa wameripotiwa kujisikia kizunguzungu na uchovu usio wa kawaida (fatigue) wawapo kwenye draya hizo.
UMEME WAKE UNAVYOATHIRI
Katika kufafanua hilo, Dr. Mwinuka alisema joto linalozalishwa na umeme kupitia draya huwa na kiwango kikubwa cha uzio wa sumaku (magnetic field) ambacho huathiri balansi ya kiwango cha umeme ndani ya mwili wa mtu aliye karibu. Madhara hayo huonekana sana kwa kina mama wajawazito ambapo moja kwa moja huwa kwa mwanamke mwenyewe na kwa mtoto ambaye yupo tumboni.
MADHARA KWA MJAMZITO
Akifafanua zaidi, Dk. Mwinuka alisema katika miezi mitatu ya kwanza, mwili wa mwanamke mjamzito unakuwa bado haujazoea hali ya kuwa na kiumbe kipya ndani ya mwili wake. Hivyo bugudha yoyote isiyo ya kawaida, mfano joto la umeme litengenezwalo na draya inapotokea, huweza kusababisha ukuaji mbovu kwa mtoto aliye tumboni na madhara mengine kama ugonjwa wa pumu (asthma) ambao huenda ukamkuta mtoto akishazaliwa.
MADHARA YA MUDA MREFU
Madhara mengine huweza kusababishwa na utaalamu mdogo wa mtumiaji ambapo matokeo yake huweza kutokea baada ya miaka mingi kupita kwa mfano uvimbe kwenye ubongo (brain tumoir) na mabadiliko ya vinasaba.
USHAURI WA BURE
Wanawake wanapoosha nywele zao, wanashauriwa kutumia vitambaa vikavu na kutumia jua la asili ili kuepuka kupata madhara mbalimbali.
No comments:
Post a Comment