CHANZO cha bainika kinachosababisha wasanii nchini kufa masikini huku wakiwa na majina makubwa ambayo yanasababisha kuzikwa kama wafalme huku wakionekana kuacha pengo ambalo haliwezi kuzibwa na mtu mwingine kutokana na uwezo wa kazi ya sanaa anayokuwa nayo.
Siku 14 zimepita tangu watanzania kupata pigo la kumpoteza msanii wao ambaye alikuwa mkali katika miondoko ya Hip Hop Albert Mangwea 'Ngwair', watanzania waliowengi walijitokeza ili kufanikisha safari ya mwisho ya msanii huyo inafanikiwa.
Baadhi ya wasanii mbalimbali walikumbwa na mshangao kutokana na mwamko wa baadhi ya watanzania kujitokeza kwa wingi katika maziko ya msanii huyo huku wao kujiona kubaki masikini.
Kutokana na hali hiyo wasanii kupoteza maisha huku wakiwa masikini na baadhi yao kushindwa kuendeleza maisha yao msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Ommy Dimpoz aeleza sababu ya chanzo hicho.
Alisema kuwa baadhi ya kampuni haziwekezi kwa wasanii nchini hivyo maisha ya wasanii yanategemea shoo ambapo ujira unaopatikana kutokana na shoo hizo haziwezi kutosha kuendesha maisha yao.
Dimpoz alieleza kuwa bado kampuni zinatakiwa kujitokeza kwa wingi katika kuokoa maisha ya wasanii wa tanzania hususani wanamuziki ili kuinua kiuchumi .
"Tumechoka kila siku kuzika wasanii maskini, tunakufa masikini huku tukiwa hatuna kitu ingawa tuna majina makubwa tunayoyaacha lakini tumeacha nini tofauti na majina yetu jibu ni hakuna" alisema Dimpoz
Mbali na hayo Dimpoz alishangaa baadhi ya kampuni kutumia masupastaa wa nje ya nchi katika matangazo yao wakati walikuwa na uwezo wa kuwatumia wao kama mabalozi ili kuwainua kiuchumi.
"Unajua nashangaa sana kampuni wanawatumia baadhi ya watu wenye majina makubwa wa nje na kuwaacha wa ndani lakini wakiwa na tamasha wanawachukua wasanii wasanii wa ndani kwa ajili ya kunogesha tamasha lao" alilalamika Dimpoz.
Wakati huo huo pia mbunge wa Mbeya Mjini kupitia chama cha (CHADEMA) Joseph Mbilinyi 'Sugu' aliweka wazi kuwa kazi za sanaa zinatakiwa zilindwe ili kumnufaisha msanii pamoja na taifa kiujumla.
Alisema ili kuepusha umasikini kwa baadhi ya wasanii serikali inatakiwa kuunda sheria za kudhibiti wizi wa kazi za sanaa ili kulinda maslahi, pamoja na hayo pia wasanii kuungana ili kutetea maslahi yao pidni wanapohitajika kufanya hivyo.
Kwa upande wake Kala Jeremiah alisema chanzo cha wasanii kufa umasikini imechangiwa na serikali kwa kusindwa kudhibiti mianya ya wizi unaofanyika katika kazi zao .
Alieleza kuwa kampuni wanatakiwa kujitoa moja kwa moja kwa wasanii na siyo kama wanavyofanya sasa kwa kumtumia mtu mwingine ambaye anatumika kama daraja la kumfikia msanii.
"Unajua utakuta baadhi ya kampuni wanatumia mtu kama daraja la kumfikia msanii matokeo yake mpaka hela inapokuja kumfikia msanii inakuwa ndogo kulinganisha na kazi wanayoifanya " alisema Kala.
Baadhi ya wasanii walitoa wito kampuni kuwekeza kwa wasanii ili kuinua vipato na kuokoa umasikini ambao unawakabili ili kuepusha vifo vya wasanii maskini huku wakiwa wanaacha majina makubwa katika jamii.
No comments:
Post a Comment